HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2011

Exim yaahidi kusaidia kuinua uchumi nchini


Na Mwandishi Wetu
Benki ya Exim imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika mikakati mbalimabli ya kuinua uchumi wa nchi.Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu wa benki hiyo, Bwana Dinesh Arora alipokuwa akizungumzia ufadhili wa benki hiyo kwenye mkutano wa uwekezaji Afrika uliofanyika jijini katikati ya mwezi huu na kuhudhuriwa na maraisi watano kutoka nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki na wajumbe zaidi ya 900 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Alisema kuwa sekta binafsi inao wajibu mkubwa wa kuisaidia serikali kuinua uchuni na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania. “Exim Benki iliona fahari kubwa kufadhili mkutano huu ambao ulikuwa una lengo la kuonyesha utajiri wa rasilimali za nchi na pia kufungua fursa za kibiashara”alisema.

Bwana Arora alisema kuwa Benki ya Exim itaendelea kusaidia fursa kama hizo ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kuweza kupata nafasi ya kukutana na wafanyabiashara kutoka sehemu nyingine za dunia.Alisema kuwa benki yake ina wajibu mkubwa wa kuendelea kuisaidia uchumi wa nchi kukua.

Alisema kuwa ili wajasiriamali wa Kitanzaniia waweze kukua kibiashara na kutoamchango mkubwa zaidi kwenye uchumi,lazima ziwepo juhudi za makusudi za kuwakutanisha na wawekezaji kutoka Afrika na duniani kote.“Tunaamini kuwa maendeleo ya benki yetu yanategemea sana mafanikio ya jamii yetu tunakofanyia kazi”alisema.

Alisema pamoja na biashara benki hiyo ina jukumu la kuchangia shughuli mbalimbali za kijamii na kwamba Ujasiriamali ni miongoni mwa sekta zinazochangiwa kwa nguvu na benki husika. “Tumekuwa tunafanya biashara ya kibenki kama jukumu letu kuu lakini pia tumekuwa na majukumu mengine kwa jamii inayotuzunguka hivyo udhamini wetu katika TEYA ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu hayo na kwamba Ujasiriamali tunauangalia kwa namna ya kipekee,” alisema Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa sekta ya hiyo,hivi karibuni wamefungua

akaunti mpya ya Tumaini maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali wanawake. Alifafanua kuwa pamoja na wengine wanawake ni mhimili mkuu wa shughuli za kijamii katika familia nyingi za kitanzania hivyo benki hiyo imeona ipo haja ya kipekee kuwawezesha ili nao waweze kumudu majukumu yao kwa ufanisi. Kuhusu tuzo hiyo alisema ni changamoto ya kutosha kwa Wajasiriamali nchini katika kuhakikisha shughuli wanazozifanya zinakuwa na tija kwao binafsi na taifa kwa ujumla.

“Akaunti ya Tumaini ni maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali Wanawake na hii inaonyesha jinsi tunavyoijali sekta hii lakini pia tuzo hii ni changamoto kubwa kwa wahusika kwani itawasukuma kufanya shughuli zenye tija,” alisema Bwana Arora. TEYA imelenga kutambua kazi za Wajasiriamali katika nyanja mbalimbali kutokana na mchango wao katika pato la taifa na ukuaji wa uchumi lakini pia kutoa changamoto ya ushindani kwa wahusika na sekta ya kibiashara kwa ujumla.

TEYA 2011 ilizinduliwa rasmi Machi 15 mwaka huu na inatarajiwa kutolewa baadaye Novemba ambapo Raisi Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad