Na Dixon Busagaga,Mombasa.
TIMU ya soka ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro imefanikiwa kujinyakulia kikombe na medali baada ya kuichapa timu ya soka ya Nairobi water bao 1 kwa 0 katika mashindano ya bonanza la Pasaka lililofanyika katika mji wa Mombasa nchini Kenya .
Katika Bonanza hilo linaloandaliwa na shirika la bandari la nchini Kenya (KPA) kila mwaka,jumla ya timu sita zikiwa katika makundi mawili, timu ya Moshi veterani ndio ilikuwa wawakilishi pekee kutoka Tanzania .
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika uwanja wa mpira miguu wa KPA,Mwenyekiti wa timu ya Moshi veterani Madesho Moye alipongeza waandaaji wa bonanza hilo kwa zawadi zilizotolewa kwa washindi.
“Nitumie nafasi hii kupongeza uongozi wa bandari kwa zawadi,tumezoea kuona zawadi kama hizi zikitolewa katika ligi kuu,na mashindano makubwa huko ulaya,lakini ninyi mkaona japo tunacheza mpira umri ukiwa umetupia tunastahili kupena vikombe na medali kwa hili niwapongeze sana”alisema Moye.
“Kwetu sisi ni heshima kubwa sana mmetuonesha sina shaka hautuna budi kuiga yote mazuri tuliyoyaona hapa KPA na kwa timu zilizoshiriki pia”aliongeza Madesho.
Moye alisema timu ya soka ya Moshi veterani maarufu kama wazee wa safari hawana budi kulingia zawadi ya kikombe na medali zilizopatikana kutokana na kwamba ni timu chache Tanzania hususani za Veterani zilizo pata mafaniko ukilinganisha na Moshi veterani.
Aidha Moye alisema lengo la kuanzishwa kwa timu ya Moshi veterani linaelekea kutimia kutokana na mpango wake wa kutaka kusaidia wachezaji wanaochipukia kupata nafasi ya kucheza soka nje ya nchi.
“Malengo yetu sisi kama Moshi veterani sasa yanaelekea kutimia kutoka na urafiki tunaoendelea kujenga baina yetu na watu mbalimbali kupitia michezo,tunao vijana ambao tunawalea wenyewe na ni wachezaji wazuri tunahakika tutawaleta waje wasaidie timu ya Bandari inayoshiriki ligi
kuu ya Kenya.”alisema Madesho.
Katika bonanza hilo mchezaji Hassan Said wa Moshi veterani pia alichaguliwa mchezaji bora ambapo alikabidhiwa zawadi ya kiatu cha dhahabu huku timu ya Moshi veterani ikipata mualiko wa mashindano mengine jijini Nairobi yatakayoandaliwa na Benki ya Bacrays.

No comments:
Post a Comment