Mh. Balozi: Jaka Mgwabi Mwambi (mwenye kofia ya baraghashea) akishiriki katika dua ya kuwarehemu marehemu ndani ya ukumbi wa ubalozi wa Tanzania Urusi mjini Moscow.
Salam bro.Michuzi,
tumai u mzima wa afya, naomba msaada wako kwa niaba ya familia ya Mh.Balozi: JAKA MGWABI MWAMBI, MKE WA BALOZI, EDDY MKALI, SULEIMAN DITOPILE MZUZURI, HASSAN HASHIMU KAPILIMA wote waishio jijini Moscow kwa kuniwekea Tangazo la HITIMA la NDUGU ZETU tuliolifanya kwa pamoja tarehe23-04-2011, katika ukumbi wa UBALOZI WA TANZANIA, RUSSIA hapa jijini MOSCOW. Tafadhali picha na maelezo yapo katika attached document in m-word.
tumai ombi langu utalipa uzito wake.
wako,
Hassan Hashimu Kapilima
Moscow
Mama Balozi (mwenye Hijab nyeusi) na kushoto kwake ni Mh.Balozi Jaka Mgwabi Mwambi akitoa shukrani kwa niaba ya familia zote za wafiwa baada ya hitima
Mh. Balozi: Jaka Mgwabi Mwambi mwenye kofia, waliokaa wa pili toka kulia akiwa katika picha ya pamoja kati ya familia za wafia, maustadhi na ndugu jamaa na marafiki walioshiriki katika hitma hiyo.
Mh. Balozi: Jaka Mgwabi Mwambi mwenye kanzu, waliokaa wa pili toka kulia akiwa katika picha ya pamoja baada ya shughuli nzima ya hitima kuisha.
No comments:
Post a Comment