HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 27, 2011

PILI HASHIM AIBUKA MISS TANGA CITY CENTRAL 2011

Hatimae mnyange wa kitongoji cha Miss Tanga City Central amepatikana huku shindano hilo likiacha historia kubwa. Mwanadada Pili Hashim ndie aliyabahatika kuvaa taji hilo ambalo hapo kabla lilikuwa likishikiliwa na Anna Kiwambo mrembo wa kitongoji hicho kwa mwaka jana. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mishi Juma huku nafasi ya tatu ikienda kwa Salha Ibrahim. Kitongoji ca Miss Tanga City Central kiliandaliwa na kampuni ya Green Apple Entertainment kwa udhamini mkubwa wa Madam Hair Dressing Saloon, Mwanakodo, Sarah Issa, Arbab MB pamoja na Anko Mo Blogspot. Warembo wanne wamebahatika kuingia kunako kambi ya Miss Tanga 2011 ambapo kwa mwaka huu inaandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment na itafanyika tarehe 11/06/2011 pale Mkonge Hotel. Kabla ya hapo Miss Tanga ilikuwa ikiandaliwa na kampuni ya Five Brothers Entertainment.
Anaitwa Anna Kiwambo, ndie aliyekuwa anarudisha taji baada ya muda wake kumalizika. Anna Kiwambo pia ndie Miss Tanga 2010.
op Five ya Miss Tanga City Central 2011....Pili Hashim (4), Rukia Shemdoe (1), Salha Ibrahim (3), Judith Kitogo (2) na Mishi Juma mwenye namba (5).
Majaji wakiwa makini wakifuatilia warembo.

kwa picha zaidi tembelea VIJIMAMBO VYA TANGA kupitia link hiyo hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad