Simu ikiwa imelipuka na kusababisha chumba kuungua moto katika eneo la Kihesa mjini Iringa leo asubuhi
Kikosi cha zima moto kikiwa kimefika eneo la tukio kujaribu kuzima moto japo kilifika kwa kuchelewa na kukuta mali zote zimeteketea Sofa na mali nyingine za afisa masoko wilaya ya Iringa, Tito Kilale ambaye pia ni mchungaji zikiwa zimeteketea kwa moto. mali zilizosalimika yakiwemo magari mawili ambayo yaliegeshwa nje ya nyumba hiyo Watoto wakiwa wamejilaza nje baada ya nyumba yao kuwaka moto kutokana na simu iliyokuwa imewekwa chaji kulipuka na kuteketeza nyumba na vitu vilivyokuwepo ndani.Tahadhari kwa watumiaji wa simu ambao wamekuwa na kawaida ya kuacha simu zikiendelea kuchajiwa kwa muda mrefu kuacha utaratibu huo kwani madhara yake ni makubwa sana.
No comments:
Post a Comment