Na Ally Changwila
Serikali ya India kuisadia Tanzania kwa kuipatia mkopo wa dola za kimarekani milioni 190 katika kutekeleza mradi wa Maji Dar es Salaam(2013), ikiwa ni sehemu ya kuendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na India.
Katika mazungumzo yake na Waziri wa Maji Prof. Mark Mwandosya ofisini kwake Ubungo jijini Dar es Salaam jana(Leo Jumapili) Mwenyekiti wa Kampuni ya OIA Infrastructure Developers, Balozi V.B Soni alisema kuwa tamko rasmi la makubaliano ya mkopo huo pamoja na utiaji saini wake, utafanywa nchini mwezi ujao na Waziri Mkuu wa India ambaye ataitembelea Tanzania.
Balozi.Sonia alisema kuwa hatua ya India kuisadia Tanzania imetokana na ukweli kwamba uchumi wao kwa sasa umekuwa na hivyo wameona nivyema na wao kuzisaidia nchi nyingine za kiafrika ikiwemo Tanzania.
Ameongeza kuwa kampuni yake ya OIA ambayo ndiyo itakuwa msimamizi mkuu wa utekelezaji wa shughuli nzima inayofanywa kupitia mkopo huo hapa nchini , amezitaja nchi nyingine za kiafrika walizozisadia katika miradi mbali mbali kuwa ni pamoja na Sudan,Congo,Ethiopia na Mozambique.
Balozi Sonia ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali kuwaikilisha India kibalozi Afrika ikiwemo nchi za Senegal, Mali,Mauritania na Guinea Bissau, amesema kuwa amefurahishwa sana na namna Tanzania inavyotekelekeza mambo mbalimbali haraka pasipo kuwa na mlolongo mrefu tofauti na nchi nyingi alizozitembelea.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mwandosya amesema kuwa mbali na msaada huo wa ujenzi wa mradi wa Maji DSM ni vyema pia kuangalia uwezekano wa kuipatia Tanzania msaada wa kuijengea uwezo.
Akiongeza katika hilo Waziri Mwandosya amesema hapo awali wataalam mbalimbali wa Masuala ya Maji waliwahi kupatiwa mafunzo nchini India, lakini sasahivi karibu wote wanaelekea kustaafu, hivyo ni vyema kuandaa utaratibu wa kuwapitia mafunzo kama hayo waajiriwa wapya wa wizara ya maji ili kuziba pengo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Christopher Sayi amweleza Balozi Sonia kuwa ni vyema taratibu za manunuzi zikazingatiwa katika mchakato mzima wa utekelezaji wa mradi huo unaotokana na mkopo huo kutoka serikali ya India.
Mbali na Waziri wa Maji na Katibu Mkuu wa wizara ya Maji, hafla hiyo fupi pia ilihudhuriwa na Kaimu Mkuregenzi wa Idara ya Maji Kibishara Bi Mary Mbowe, Mkurugenzi wa DAWASA Bw. Arcard Mutalemwa, Mwakilishi kutoka Idara ya Sera na Mipango Bw.Mwinyiheri Ndimbo, Katibu wa Waziri Bw.Ngusa Izengo ,Afisa Habari Bw. Ally Changwila na Bw.Painento Makweba kutoka Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Na kwa upande wa ugeni wa kutoka India pia alikuwepo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya OIA Bw. Udayan Murkherjee na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bw.Tripurari Goyal.

No comments:
Post a Comment