
Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea udhamini wa tuzo za mwanamichezo bora wa Tanzania, uliotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wa kiasi cha sh. milioni 80 kwa ajili ya maandalizi ya tuzo hizo hizo zitakazofanyika Mei 6 mwaka huu.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mapunda.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 80 kwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (kushoto) katika hafla iliyofanyika mchana wa leo katika hoteli ya Movenpick jijini Dar.Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA,Maulid Kitenge (pili shoto),Meneja Mahusiano wa SBL,Nandi Mwiyombella (kati) na Katibu Mkuu wa TASWA, Ameir Mhando.
No comments:
Post a Comment