HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 21, 2011

Mwandosya ahofia hali ya upatikanaji maji ZiwaTanganyika

Waziri wa Maji Prof.Mark Mwandosya(wa pili kushoto) akifanya mazungumzo na Mtaalam anayeshughulikia Rasilimali za Maji kutoka Benki ya Dunia Bw,Rafik Hirji (kushoto) ofisini kwake Ubungo jijini Dar es salaam.Mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika nia ya kufanyika tafiti kwenye ziwa Tanganyika na hali ya upatikanaji wa Rasilimali za maji katika eneo hilo.wengine pichani ni baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo.

Na Ally Changwila

Waziri wa Maji Prof Mark Mwandosya amesema upo umuhimu wa kutafuta suluhisho la haraka kuhusiana na hali ya kupungua kwa upatikanaji wa rasilimali za maji katika bonde la Ziwa Tanganyika badala ya kujikita kwenye suala kubwa la mabadiliko ya Tabia nchi ambalo ni eneo pana na la muda mrefu.

Waziri Mwandosya ameyasema hayo ofisini kwake Ubungo jijini Dar es salaam jana wakati alipokutana na mtaalam anayeshughulikia Rasilimali za Maji kutoka Benki ya Dunia Bw.Rafik Hirji, na kuongeza kuwa mbali hilo pia hivi sasa kuna upungufu wa vituo vya kukusanya takwimu za rasilimali ya Maji na kushauri pia kuwepo na ongezeko la kutosha la vituo vya kukusanya takwimu.

Waziri Mwandosya pia amegusia pia haja ya kufanya ukarabati wa kituo cha Lukuga ambako kitolea maji chake Kimebomoka.

Waziri Mwandosya amesisitiza kuwa kama hayo yatazingatiwa na kufanyika ipasavyo,itasaidia hata kurahisisha pale inapokuja katika kuangalia suala la mabadiliko ya Tabia nchi kwa ujumla kwa kuwa kutakuwa na takwimu za kutosha.

Awali Bw. Hirji alimwelezea Waziri Mwandosya ,kuwa Benki ya Dunia imezingatia mazungumzo yake ya awali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia ambako Waziri Mwandosya aliomba kupatikane fedha kwa ajili ya kufanya tafiti katika ziwa hilo.

Bw.Hirji amesema jitihada zinafanywa na Benki ya Dunia kuwasiliana na taasisi mbalimbali ili kupatikana na fedha za kufanya utafiti katika Ziwa Tanganyika ili kuweza kujua tatizo la chanzo cha kupungua kwa kina cha maji katika eneo hilo na Benki ya Dunia ipo tayari kuhakikisha fedha zinapatikana kwa tafiti hizo.

Bw.Hirji aliongeza kuwa tayari Taasisi ya mazingira ya Dunia (GEF) imeshaonyesha nia ya kusaidia , na kuongeza kuwa suala la rasimali za maji katika eneo la Ziwa Tanganyika sio la ki nchi pekee bali ni suala mtambuka na linazigusa nchi kadhaa zinazopitiwa na Ziwa hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad