
Mkuu wa Kituo kinachoshughulika na Uangalizi wa Vituo vya Ukombozi kilichoko Nchini Namibia,Dkt. Ndahafa Nghifindaka Kulia pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Habari Ajira Utamaduni na Michezo wakiangalia KIsima kisichokauka wala kujaa na hutumiwa na watu kama maji ya baraka ya kuombea dua wakati wa matatizo kilichoko Kaole Ruins mjini Bagamoyo Mkoani Pwani leo.

Muelezaji wa Kaole Ruins kutoka Wizara ya Utalii na Mali Asili akielezea ujumbe ulimsindikiza Mkuu wa Kituo cha Ukombozi kutoka Namibia Dkt. Ndahafa Nghifindaka wa pili kushoto makaburi ya zamani yaliyoko Kaole Ruins mjini Bagamoyo Mkoani Pwani leo.

Mkuu wa Kituo kinachoshughulika na uangalizi wa Vituo vya Ukombozi wa Afrika kilichoko Nchini Namibia Dkt.Ndahafa Nghifindaka kulia na kushoto ni Mtafiti na mwandishi Historia za Ukombozi Bwana Simeon Angombe wakiangalia Ukumbi ulitumiwa na wapigania Uhuru wa Afrika ulioko Kaole ambayo ni Shule ya Sekondari ya Wazazi iliyoko mjini Bagamoyo Mkoani Pwani leo.

Dkt Ndahafa nghifindaka alievaa nguo ya kitenge kutoka Namibia pamoja na ujumbe uliomsindikiza wakiangalia kaburi la mke na mume (Wapendanao), Kaburi hili wamezikwa mume na mke waliokufa siku moja kwa ajali katika Bahari ya Hindi na kuzikwa kwa pamoja kaburi hili liko Kaole Ruins mjini Bagamoya Mkoani Pwani.Picha na Anna Itenda -Maelezo.
No comments:
Post a Comment