Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo (pili shoto) akiwa pamoja na viongozi wakuu wa mchezo wa Darts hapa nchini,toka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Darts Taifa,David Msabi,anaefuata katikatini ni Mwenyekiti wa Darts Taifa,Gesase Waigama,Katibu Mkuu wa Darts Taifa,Mohamed Bitegeko pamoja na Katibu Mkuu wa Darts mkoa wa Dar es Salaam,Lambati Rwihula.hapa walikuwa wakifuatilia baadhi ya wachezaji wa mchezo huo wa Darts toka nchi tatu za Afrika Masharizi wakijifua kujiandaa na mashindano ya mchezo huo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi kesho katika ukumbi wa Moshi Bar,Manzese Tiptop.
Mwanamama wa kitanzania toka Mkoani Arusha akionyesha umahiri wake wa kucheza Darts leo.
Mwanadada kutoka nchini Kenya nae hakuwa nyuma kuonyesha umahiri wake katika mchezo ambao utaanza kutimua vumbi kesho katika ukumbi wa Moshi Bar,Manzese Tiptop.
Baadhi ya wachezaji wa Darts wanaounganisha nchi tatu za Afrika Mashariki (Tanzania,Kenya,Uganda) wakiendelea kujifua katika ukumbi wa Moshi Bar Manzese Tiptop leo.
No comments:
Post a Comment