HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 22, 2011

KAMERA YA MTAA KWA MTAA NA MATUKIO YA JIJINI DAR LEO

hapa ni kwenye mzunguko wa raundi abauti ya mtaa wa Uhuru na Msimbazi,ambapo kwa wenye magari hupiata katika eneo hilo kwa kuzidiana ujanja na si kwa kufuta sheria za barabarani.
Mtaa wa Msimbazi mara baada ya mvua kunyesha.
Msela akijibebea mahindi yaliyokuwa yamehifandiwa pembeni na mchomaji wa mahindi ambaye alikuwa bize na biashara yake.
Wazee wa Bodaboda wakisikilizia vichwa kwenye kona ya Uhuru na Msimbazi,haya jamaa siku hizi wamepanda chati kama nini kiasi kwamba hata madereva taxi hawafanyi kazi tena kama zamani.
Kuelekea Kamata....
Kituo cha Daladala cha Mwembechai kinavyoonekana leo huku kikiwa kimependezeshwa na matairi chakavu katika chemba zilizoibiwa mifuniko yake.
Ile ya chuma wanaiba kwa madau ya vyuma chakavu,na hii nayo wanafanyaje???

1 comment:

Post Bottom Ad