Mshindi wa mwaka jana Zahra Selemani ambaye alinyakua taji la Miss Arusha City Center 2010.
Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2011 yanatarajiwa kufanyika mei 13 mwaka huu katika ukumbi wa Club ya Tripple A, jijini Arusha.
Akizungumza na Ripota wa Blogu yetu hii, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa kwa sasa wamejiandaa vyema na wako tayari kwa ajili ya kufanya mashindano hayo.
Shindano hilo linalotarajia kufanyika jijini Arusha hapo mei 13 tayari mpaka sasa wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu anatokea mkoani Arusha.
"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.
Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.
No comments:
Post a Comment