Nahodha wa Timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akiwa kwenye gari la wazi huku akiwa na mwali wao mara baada ya kuwasili jijini Dar mchana huu.

Msafara wa Kutoka uwanja wa Ndege wa J.K Nyerere kuelekea klabuni kwao ukianza.

Kocha mkuu wa Timu ya Yanga,Sam Timbe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere kutokea jijini Mwanza walikokuwa wameenda kucheza mchezo wao wa kumalizia ligi kuu na kuunyakua ubingwa wa ligi hiyo kwa mwaka 2010/11.

Nahodha wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa (FUSSO) akiongea na vyombo vya habari juu ya ubingwa walioupata huko jijini Mwanza jana,katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere mchana huu.


Baadhi ya wachezaji na viongozi wa Yanga wakitoka uwanjani hapo kuelekea kwenye magari yaliyoandaliwa kwa ajili ya safari ya kwenda klabuni.

Mdau Ellihuruma Ngowi wa Vodacom akiwa na mwali huyo mchana huu.

Mashabiki wakilazimisha kumsaidia kombe nahodha wao,Shadrack Nsajigwa katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere mchana huu.

yaani ni furaha mtindo mmoja kwa mashabiki wa timu ya Yanga.

Msafara.

Mapokezi yakiwa yamepamba moto.
inaonekana yanga wametua dar na kombe mkononi sasa haya makombe yako mawili au ndo mshindi alishatabirika?.......hongera yanga ila mchezo wa kungojea matokeo si issue ndo maana boli la bongo linasuwa..........ushabiki maandazi wa TP Mazembe akicheza na mbongo then unamuunga mkono mgeni si ishu ni ushamba
ReplyDeletemkereketwa