
Kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars, Jan Poulsenn akizungu mza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati alipokuwa akikitangaza kikosi cha wachezaji 19 kitakachoivaa timu ya Msumbijini.
Na Mwandishi wetu.
Kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 19 kitakachoivaa Msumbiji huku akiwaongeza Kigi Makasi na Amir Maftah na kumuacha mlinda mlango Juma Kaseja katika msafara wa Msumbiji.
Poulsen alisema kuwa kikosi hicho kitaingia kambini Aprili 15 kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Msumbiji utakaochezwa Aprili 23 na kwamba ameamua kuwaongeza Kigi Makasi na Amiri Maftah kutokana na uhodari wa wachezaji hao kuwa viraka kwani wanauwezo wa kupanda na kushuka kama mabeki wa kulia.
Alisema amemuacha mchezaji Stephano Mwasika kutokana na kuwa majeruhi na kudai kuwa Kaseja atamjumuisha kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya CAN.
Poulsen alisema kikosi hicho kitacheza na Bafanabafana Mei 14 na kwamba mara baada ya mechi ya Msumbiji timu hiyo itapumizika kwa wiki mbili na kuingia tena kambini May 2 kujiandaa na mechi hiyo ya Bafanabafana.
Alisema mara baada ya mechi hiyo ya Bafanabafana Mei 14 kikosi chake kitapumzika siku mbili na Mei 17 kitaingia tena kambini kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Afrika ya Kati.
Alitaja wachezaji watakaocheza mechi ya Msumbiji ni Makipa ni
Shaban Kado (Mtibwa) na Shaban Dihele (JKT Ruvu).
Safu ya Ulinzi: Shedrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub 'Canavalo' (Yanga), Amir Maftah (Simba), Juma Nyoso (Simba), na Kigi Makasi (Yanga).
Viungo Nurdin Bakari (Yanga), Shaban Nditi (Mtibwa), Jabir Aziz (Azam), Ramadhan Chombo 'Redondo' (Azam), na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).
Washambuliaji Salum Machaku (Mtibwa), Mrisho Ngassa (Azam), Mohamed Banka (Simba), John Bocco (Azam) na Mbwana Samata (Simba).
Pia kocha huyo raia wa Denmark alisema wachezaji wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi watajiunga na wenzao Mei 17 akiwemo Kaseja wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi ya Afrika ya Kati ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na ameamua kutowaita hivi sasa kwa vile mechi wanazocheza nazo ni za kirafiki.
Wachezaji hao ni Juma Kaseja (Simba), Idrissa Rajabu (Sofapaka), Henry Joseph (Kongsvinger IL Norway), Abdi Kasim, Danny Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden).
No comments:
Post a Comment