HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 14, 2011

TBL YAKARABATI ZAHANATI YA KIVULE

Mkandarasi wa Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Doris Malulu (kulia) wakijadiliana jambo na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kivule, Sophia Nkokoo walipotembelea juzi kukagua ukarabati wa Jengo la wazazi unaofanywa kwa msaada wa TBL, baada ya kuharibiwa na bomu lililotokea Kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, mwezi uliopita. TBL imetoa sh. mil 30 za kukarabati jengo hilo na kununua vifaa vilivyoharibiwa.
Mkandarasi wa Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kulia) akitoa maelekezo kwa Fundi Mwashi Rajab Nesto alipokuwa akikagua ukarabati wa jengo la uzazi la Zahanati ya Kivule unaofanywa kwa msaada wa TBL, baada ya kuharibiwa na bomu lililotokea Kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, mwezi uliopita. Mwingine nI Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Doris Malulu. TBL imetoa sh. mil 30 za kukarabati jengo hilo na kununua vifaa vilivyoharibika.
Mkandarasi wa Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Doris Malulu wakikagua ukarabati wa Zahanati ya Kivule unaofanywa kwa msaada wa TBL, baada ya kuharibiwa na bomu lililotokea Kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam, mwezi uliopita.TBL imetoa sh. mil 30 za kukarabati jengo hilo na kununua vifaa vilivyoharibika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad