Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Slaa akiwa ndani ya gari aina ya Iveco Euro Cargo ikiwa ni moja kati ya magari matatu ya kubebea taka ngumu pamoja na vifaa maalum vya kuhifadhia taka hizo vilivyonunuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi wake,shughuli hii imefanyika mapema leo asubuhi ndani ya yadi ya kampuni ya INCAR Tanzania iliyopo Pugu Road.Magari hayo pamoja na Vifaa hivyo vya kuhifadhia taka vimegharimu kiasi cha shilingi mil. 800.
Kifaa kikipakiwa garini.
Foko Lifti ya INCAR Tanzania ikiweka sawa moja ya kihifadhia taka ngumu kati ya 38 vilivyonunuliwa na Halmashauri ya Ilala kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi wake.
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Slaa (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Halmashauri ya Ilala pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya INCAR Tanzania mapema leo asubuhi wakati walipokwenda kuchukua magari hayo.
No comments:
Post a Comment