HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 27, 2011

tamasha la upendo la KKKT lafanyika jijini dar

Kikundi cha kwaya kutoka Magomeni kikiwasha moto katika Tamasha la Upendo lililokuwa limeandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania-KKKT usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangisha hela ya kuwawezesha wanakwaya hao kwenda mjini Mbeya kutoa huduma na zawadi kwa watoto yatima.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania- KKKT (wa pili kulia), Alex Malasusa ambaye alikuwa mgeni akifuatilia tamasha hilo.
Wachungaji wakifuatilia Tamasha la Upendo
Hapa ni kazi tu!, inaonyesha jinsi mwanamama wa kwaya kutoka Magomeni anavyochalaza....
Barnaba akiwa upande wa pili yani hapa namaanisha akivurumusha mapambio na nyimbo za dini kwenye Tamasha hilo.
Kikundi cha Voice wakifanya vitu vyao katika tamasha hilo la injili lililopewa jina la Upendo.
Hawa ni viongozi wa Kwaya ya KKKT-Azania Front wakijadiliana jambo, kutoka kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo, Michael Nkya, Mjumbe Emanuel Sanare, Mwalimu wa Kwaya Godfrey Moshi pamoja na Mwenyekiti wa Maandalizi
Kikundi cha wanakwaya cha KKKT-Azania Front kikitoa burudani jioni hii.

1 comment:

  1. ..Duh mbona hao waandaji wote wachaga kuna usalama kweli hapo?????

    ReplyDelete

Post Bottom Ad