Mambo vipi Mzee wa Kitaa Kwa Kitaa??
Hebu niwekee hii kitu ili wanalibeneke waweze kuchangia mada hii.tangu nimepata akili timamu nimekuwa nikisikia kwamba, eti wabongo walio wengi huko mbele (Ulaya na kwingineko) eti hufanya kazi kama hii aifanyayo huyu mzee hapa pichani (KUZIBUA VYOO) na nasikia wanawin kinoma maisha tena ile mbaya.
Sasa kama ni kweli inalipa mbona hawaonyeshi huo uzalendo hapa Nyumbani pindi wakirudi ili wawe mfano kwa wengineeee?????Naomba tusaidiane kueleweshwa katika hili tafadhali.
Mdau wa Kitaa Kwa Kitaa huku kwetu.
ndugu yangu hakuna mbongo anafanya kazi hizo ulaya usidanganywe hizo kazi zinawenyewe na zinalipa kiukweli nikazi za wenye nchi hata hivyo kwa sasa kazi ulaya na kwengineko hazipo tena hata hizo za kubabaisha tulio huku tunasoma ndio tunawaona wanavyo angaika hakuna naisha huku na hao wabongo wanao fanyakazi huku sio hizo na nikazi za ujanja ujanja tu nawengine wanapenda kurudi home wanashindwa kwa aibu maana atarudi huko hana mbele wala nyumma matokeo yake aanze kuomba nauli hata ya magomeni kariakooo ndiomaana wanaamua wafie hukuhuku
ReplyDeleteUmesema Ukweli mdauu hapo juu hata mie nakuunga mie pian ipo huku... Kazi kama hizo watu wanatumia vifaa na vitu vya kujikinga siwezi kusema hazipo zipo ila wanafanya kwa uangalifu na kuzungushia isije kuwaharibia wengine... Zinatumia Ujuzi sio wanafanya wanatizama Afya ya mtu na Usalama... Jengine sasa hivi kazi nyingi hakuna Ulaya watu wanafikiria kurudi kama hujasoma Bongo hatari na Ulaya sasa hivi Hatari... Ila Tanzania lazima wawe wazalendo kwa watu wao kuwapa Vifaa vya utendeo kazi. Elimu ni kitu kizuri kwa binadamu ila pia tusizarau kazi za watu watu wa kuzarauliwa ni wale wauza unga na wizi na Mafisadi ndio wakuzarauliwa si Mbeba gunia au Mbeba Box... Kazi haramu ndio hazifai. KZ
ReplyDeleteNikweli hamna mbogo au mtu mweusi anaefanya kazi hizi kwani zinalipa vizuri ni wenyewe wazangu dnio wanazipata wewe mbogo ukienda kuomba mtu mweusi akiomba hapati lakini kusema weusi wabongo hawafanti kazi siyo kweli wanafanya tena nzuri kama unaelimu yako na hata kama huna elimu basi zipo kazi za magodaun ambazo zinalipa vizuri ila watu ambao hawana kazi ni wavivu hata wangekuwa bongo akipewa kazi hatofanya au wale ambao hawana vibali au makaratasi ya kuishi katika nchi hizo za Ulaya kwa maisha yao ni magumu siyo kila mbongo anamaisha magumu, mimi nafanya kazi nzuri na nnakuja nyumbani na familia yangu kila mwaka ua kila baada ya miaka miwili kuwaona jamaa na kuwasaidia wenye kuhitaji msaada
ReplyDelete