HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 19, 2010

WADAU WA REACH OUT, SPEAK OUT AND FIGHTING HIV/AIDS TOGETHER WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA LEO

sehemu ya nyumba inayotumiwa na watoto wa kituo hiki.
Wadau tukielekea katika kituo cha kulelea Watoto Yatima na wale wasiojiweza cha Friends Of Don Bosco kilichopo maeneo ya Kimara Suka mchana wa leo,toka kushoto ni David,Nixon,Michael MX,Abubakar,Rihama na Mie.
Mmoja wa walezi katika kituo hicho,Bw.Musa Ingezi akiwakaribisha wadau wa kikundi cha REACH OUT, SPEAK OUT AND FIGHTING HIV/AIDS TOGETHER kilichopo ndani ya mtandao jamii wa Facebook waliofika kukitembelea kituo hicho mchana wa leo.
Kiongozi wa msafara wa kutembelea kituo hicho,Bw. David Ndaiga akitoa utambulisho wa ujumbe alioongozana nao kufika kituono hapo.

Baadhi ya watoto wa kituo hicho wakifuatilia kwa makini utambulisho wa wageni wao.
Rosemary Johaness akikabidhi box moja la sabuni ikiwa ni sehemu ya misaada mbali mbali iliyotolewa na kikundi cha REACH OUT, SPEAK OUT AND FIGHTING HIV/AIDS TOGETHER kilichopo ndani ya mtandao jamii wa FaceBook,kwa Mlezi wa kituo hicho Bw. Misa Ingezi.
Mweka hazina katika kikundi hicho,Elsi Sebastian akikabidhi fedha zilizochangwa na wadau mbali mbali waliopo katika kikundi hico ili kuwasaidia watoto wasiojiweza na wale wanaoshi katika mazingira magumu waliopo katika kituo hicho cha Friends Of Don Bosco,kilichopo Kimara Suka,kwa mlezi wa Kituo hicho.
Mwanamitindo,Rihama Burhan akiwakabidhi baadhi ya watoto wa kituo hicho mifuko yenye pea kadhaa za kandambili ikiwa ni sehemu ya misaada hiyo.
Wadau wa kikundi cha REACH OUT, SPEAK OUT AND FIGHTING HIV/AIDS TOGETHER wakiwa matika picha ya pamoja na baado ya watoto wa kituo hicho wakati wa kukabidhi misaada hiyo leo.
Burudani ya Mg'anda ilikuwepo huku na wengine kuvutiwa nayo mpaka kuingia kati kuonyesha uwezo wetu.
Sehemu ya misaada iliyokabidhiwa leo.
Rosemary akiwatia moyo na matumaini makubwa watoto wa kituo hicho ili wasijione kuwa ni wapweke,kwani hii ni moja ya njia katika maisha na ipo siku kila mtu atafanikiwa.

1 comment:

  1. Dah!! Pongezi sana kwenu nyote mliojitokeza! Nimevutiwa sana hadi najisikia vibaya sikuwepo!! Tuendeleze jitihada hizi jamani!
    Nafurahi kuwaona marafiki zangu kama Rihama, Elsy walikuwepo! Wow!!Nazidi kuwapenda na kuwaheshimu!
    Othman, kazi nzuri,tupo pamoja.
    X-mass hii nipo tayari kushiriki nanyi kama kuna mpango wowote.
    Taji

    ReplyDelete

Post Bottom Ad