HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 19, 2010

Libeneke La Waosha Vioo Vya Magari Barabarani

Habari Mzee wa Mtaa Kwa Mtaa,

Natumai uko poa kabisa na libeneke linasonga kama kawa,kaka hebu nisaidie kuniwekea hii kitu katika blog yetu ya Mtaa Kwa Mtaa ili wadau waweze kutoa maoni yao inshu yenyewe ni kuhusu hawa vijana wanaoosha vioo vya magari kwenye makutano ya barabara zetu. Mfano mzuri ni pale ubungo.

Hawa vijana najua wanatafuta riziki lakini badala yake wamekuwa ni kero, kwani huja tu nakuaanza mwagia maji na kufuta kioo cha gari wakiwa nalengo la kupata ujira. Si vibaya, ila matatizo yanakuja pale unapokuwa hauna hata Sh 100/= ya kumpa na kuanza kupiga gari kwa hasira na kung’oa site mirror au kufanya uharibifu wa aina yeyote ile.

Mbaya zaidi hivi sasa wamefungua kama group yao na maskani yao katikati ya barabara. Na pindi unapomwambia usioshe kioo, huwa ni vitisho vya kufanyiwa uharibifu. Sasa je hivi kweli hilo halijaonwa na wahusika? Au litafumbiwa macho mpaka lini?

Aksanteni!

Mdau niliekutana na Dhahama hii

3 comments:

  1. Poleh Mdau!Ila nina jamaa yangu ilimkuta pale Ubungo alimwambia usioshe akaosha akawaha hna Coins u know wat is follow next walitoa wiper ya nyuma ya gari wakakimbia.Nadhani Hawa wanajiita Mgambo wa jiji kutwa kuhangaika na Machinga nadhani wangeshughulikia na hawa ili to KEEP DA CITY CLEAN

    ReplyDelete
  2. Kakakkaka mie cjui hata nisemeje kuna mmoja pale Fire ukimnyima anakutukana mpk utajuta na kuna mwingine Mapipa ukimwambia sina hela kaja na style mpya analia ndo gear yake...Hili swala ni tatizo kubwa...Lukuvi na Wakurugenzi jiji mpoooooooooooo?

    ReplyDelete
  3. Kakakkaka mie cjui hata nisemeje kuna mmoja pale Fire ukimnyima anakutukana mpk utajuta na kuna mwingine Mapipa ukimwambia sina hela kaja na style mpya analia ndo gear yake...Hili swala ni tatizo kubwa...Lukuvi na Wakurugenzi jiji mpoooooooooooo?

    ReplyDelete

Post Bottom Ad