*****************************************************************
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
12/3/2010, Dar es salaam.
Serikali imeuagiza uongozi wa kiwanda cha Karibu Textile Mills (KTM) kilichoko Mbagala jijini Dar es salaam kukamilisha haraka ujenzi wa mtambo wa kusafishia maji taka utakaomudu kusafisha wastani wa lita milioni mbili ambazo hutoka kiwandani hapo kila siku.
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es salam na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira ) Dkt Batilda Burian wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya kiwandani hapo sanjari na kukagua maendeleo ya urekebishaji wa miundombinu inayotumika kutiririsha maji machafu.
Ameuambia uongozi kiwandani hapo kuwa mbali na upataji wa faida kutokana na uzalishaji unaofanyika kiwandani hapo ni vema maisha na usalama wa Binadamu na viumbe wegine ukapewa kipaumbele na kuwataka kuwa makini kwa kutohatarisha mazingira ya wananchi wanaoishi maeneo ya jirani .
“Leo tukipata faida kwa kutozingatia masuala ya kimazingira ambayo yatahatarisha maisha yetu na kizazi kitakachokuja haitakuwa inatusaidia chochote na tutakuwa tunaendelea kuathiri maisha ya watoto na akina mama wanaoishi mazingira ya jirani na viumbe wengine na ndio maana serikali tumekuwa wakali katika hilo”amesisitiza.
Amewataka viongozi wa kiwanda hicho ujenga mahusiano mazuri na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani kuliko kuendeleza migogoro ambayo inaweza kuepukika iwapo watatii sheria za nchi.
Hata hivyo Waziri Burian ameonyesha kuridhishwa na baadhi ya hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa na kufanywa na wataalam elekezi katika kiwanda hicho kuondoa tatizo la utiririshaji wa maji machafu.
Kwa upande wao viongozi wa kiwanda hicho wakiongea kwa nyakati tofauti wamesema wanaendelea kushirikiana vizuri na viongozi wa eneo hilo pamoja na wananchi wanaoishi katika eneo ili kuhakikisha kuwa hali ya usafi katika eneo hilo pamoja na utoaji wa elimu vinapewa kipaumbele.
Naye Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji - NEMC Dkt. Robert Ntakamulenga amesema tayari wameshatoa agizo kwa uongozi wa kiwanda hicho kukamilisha haraka iwezekanavyo makubaliano yote yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ikiwemo ukamilishaji wa ujenzi wa mtambo wa kusafishia maji taka kiwandani hapo.

No comments:
Post a Comment