HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 19, 2010

Semina Ya Mawakala Wa Miss Tz Kufanyika Machi 22


Semina ya mawakala wa Miss Tanzania imepangwa kufanyika Machi 22 kwenye ukumbi wa hoteli ya Giraffe hoteli jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema kuwa simina hiyo ya siku mbili ina lengo ni kuwapiga msasa waandaaji na kuwakumbusha sheria na taratibu mbalimbali za mashindano hayo.

“Washiriki wote wa semina watatakiwa kuripoti katika Hoteli ya Giraffe tarehe 22 Machi saa 2:00 asubuhi na watagaramiwa kila kitu ikiwemo chakula na malazi.” alisema Lundenga

Alisema mawakala kutoka mikoani watatakiwa wawe wamewasili jijini kufikia Machi 2.

Lundenga alisema msasa watakaopigwa mawakala hao ni kuhusu masuala ya uongozi na miiko yake, maendeleo ya sanaa ya urembo Tanzania ikiwa ni pamoja na kanuni, sheria na taratibu za mashindano ya Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2010.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad