HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 12, 2010

KKKT Kuanzisha Chuo Kikuu Kipya,Michango Yahitajika Kufanikisha Chuo Hicho

Mjumbe anaesimamia michango midogomidogo Bw. Charles Mwijage akimwonesha tv, itakayotolewa wakati wa uchangiani wa harambee, Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Eliasa Bubelwa Dar es salaam jana.
Askofu wa KKKT Dayosisi kuu ya Magharibi Elisa Bubelwa akichangia kwa njia ya simu wakati wa uzinduzi wa harambee ya kuchangia uhanzishwaji wa chuo kikuu cha joshua Kibira kilichopo Bukoba Dar es salaam jana.

*****************************************
Na Mwandishi wetu
KANISA la Kilutheri Dayosisi ya Magharibi mjini Bukoba,limewataka watanzania kuchangia gharama za uanzishwaji wa chuo kikuu mjini humo kitakachofahamika kwama Joshua Kibira University College (JoKUCo).

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa kamati ya uwanzishwaji wa chuo hicho,Bw.Moses Kagya alisema chuo hicho kitagharimu sh.bilioni 1.3 ili kukamilika na kuanza kutumika.

Bw.Kagya alisema kuwa kuwa wananchi watachangia fedha kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) ambapo mchangiaji atatakiwa kutuma ujumbe wenye neno 'Mchango' na kutuma kwenda namba 15787.

Alisema ujumbe huo utagharimu sh.350 ambapo namba za simu za wachangiaji zitaingizwa katika droo itakayochezwa kila alhamisi Mlimani City katika duka la Game na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali.

Aliongeza kuwa Chuo hicho kinatarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza Oktoba mwaka huu na kitafundisha masomo ya Ualimu,Biashara na Teknolojia (IT).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad