HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 14, 2010

Hongera Simba SC Kwa Kunyakua Ubingwa

Wachezaji wa timu ya Simba wakimbeba juu juu kocha wa timu hiyo,Mzambia Patrick Phiri mara baada ya kumalizika kwa mpambano kati ya timu hiyo ya Simba na Azam FC uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar na kuitangazia ubingwa timu ya Simba baada ya kuifunga timu ya Azam Fc kwa mabao 2-0 na kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika michezo iliyobaki, hivyo Simba inatawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2010/2011.

Kwa kweli timu ya Simba ilistahili kabisa kunyakua ubingwa huu kwani ilikuwa imejiweka vizuri sana katika msimu tofauti kabisa na mahasimu wao Yanga Sc ambao wao walianza ligi kwa kusua sua sana.hivyo sina budi kutoa pongezi zangu zilizo zadhati kabiwa kwa timu hii ya Simba SC iliyo na makao yake pale mtaa wa Msimbazi.kama nawaona vile kina Mroki Mroki,John Bukuku,Clifold Ndimbo,Mdau Pazi na wengine kibao ambao ni wanazi wakuu wa chama hili na Wekundu wa Msimbazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad