HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 9, 2010

Hali Ilivyokuwa Jijini Dar Leo

Barabara ya United National Road ilivyoshona mara baada ya Mvua ya kama guduria mbili hivi kupiga.
jamaa akiangalia gari yake kwa machungu mara baada ya pasi ya kiaina kuipitia huku Trafiki wa kujitolea akibaki kushangaa tuu na asijue la kufanya.
Hawa woote wanataka kupita katika kale ka uchochoro ka pale Upanga,mbele tu ya Makao makuu ya Jeshi la Wananchi kama unataka kutokea pale Palm Beach.yaani ilikuwa ni full shida kupita hapo.
hawa woote wamekimbilia huku ili kukwepa foleni ya barabarani.
????????????????
hadi huku mtaani kwetu nako kulikuwa hivi mara baada ya kamvua ka kiaina.sijui hii mvua ilikuwaje leo maana Jua kali kweli lilikuwa linawaka na hapo hapo bonge na la mvua nalo likashuka,mpaka nikakumbuka ule usemi usemao "ukiona jua linawaka na mvua inanyesha,basi ujue kuna Simba anazaa" sasa sijui hii hali ilikuwa ni ya kweli??

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad