HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 21, 2009

kibaka aponea chupu chupu,chuo cha CBE

Mambo vipi Othman,
Natumai uko poa na unaendelea vyema na shughuli zako za kusaka shilingi za kigongo,katika pita pita zangu za huku na huko,nilibahatika kupita pale chuo cha Biashara pale CBE na kukutana tukio la kibaka huyu alietaka kumuibia mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,lakini kwa bahati mbaya au nzuri jamaa hakufanikiwa kabisa kuchukua mali ya mtu na kutoka nayo nduki,bali alifanikiwa kuchukua mali ya mwanafunzi huyo na kuishia mikononi mwa wadau wenye hasira kali pindi wasikiapo jina la Mwizi.maana alikula kipondo cha ukweli kiasi kwamba alishindwa hata kuamka hapo mahala alipokaa.baada ya kuja askari Polisi kuokoa maisha yake.sasa sijui alisahau kuwa pale waliopo wote ni wanafunzi?maana hawana hela sasa alienda kuiba nini?...
Mdau wa Mtaa Kwa Mtaa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad