
Bwana harusi Joseph Daudi pamoja na Mkewe Maria,wakionyesha tabasamu zito mara baada kufunga pingu za maisha katika kanisa la Lutheran,Tabata na baadae sherehe ilifanyika katika ukumbi wa holi la JK,Pale Lamada Hotel,Ilala

Maharusi pamoja na wapambe wao wakiwa meza kuu ya high table,usiku huu katika ukumbi wa JK holi uliopoa Lamada Hotel.

Nyakati za mnuso ziliwadia na Bi Harusi ndie aliefungua shughuli hiyo ya mnuso.

wageni waalikwa mabibi kwa mabwana wakiwa ndani ya ukumbi wa JK holi usiku huu.

wataalam wa kufungua Shampen kutoka mamtoni nao hawakuwa nyuma katika kufanikisha shughuli hii ya bwana Joseph Daudi.

Msema Chochote (MC) mkali kuliko woote Bongo,MC Dr. Cheni,akiendeleza libeneke lake kama kawa katika kufanikisha sherehe ya bwana Joseph Daudi inakwenda kama ilivyopangwa.

mpuliza mdomo wa bata toka kundi la Mzee Hoza akifanya vitu vyake.

Vijana wa Mzee Hoza wakiendeleza libeneke kama kawa.

mduara kama kawa.

kutunzwa kwa Mama wa bwana Harusi.

picha ya pamoja ya kumbukumbu kati ya Maharusi na Wazazi.

picha ya pamoja ya wanakamati na maharusi.

mie na MC Dr. Cheni ambae leo ndie alieingoza shughuli hii ya Bwana Joseph na Bi Maria,katika ukumbi wa JK Holi pale Lamada Hotel.Dr Cheni ni moja kati ya Ma MC mahiri na wachapakazi sana hapa Bongo,hivyo kama unashughuli yako yoyote ile waweza mtwangia kwenye namba yake ya kilonga longa ambayo ni
0713 620 865,utakuwa umefanikisha shughuli yako kama utakavyotaka iwe.pia nami napenda kutoa shukrani kubwa sana kwa yule dobi wa pale Magomeni kwa msaada wake wa suti hii niliyotinga leo,nakushukuru sana Mzee na nakuombea usije bumbulukiwa na wateja wako ili uendelee kuwa na moyo huo huo wa kuniazima hizi suti maana huwaga zinantoa chicha kweli kweli kwenye hii minuso.nakushukuru sana.
Mmetoka chicha!
ReplyDeleteLeila