HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 22, 2009

Mama Nasma Khamis Kidogo Aaga Dunia


Mwimbaji maarufu wa muziki wa taarab nchini,Mama Nasma Khamis Kidogo(pichani),hatunaye tena.Mama Nasma Khamis ambaye alitamba kwa vibao kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na 'Mambo iko Huku' pamoja na Sanam la Michelin alipokuwa na Muungano Cultual Troupe, amefariki dunia katika hospitali ya Temeke usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa kwa muda na ugonjwa wa moyo.


Mipango ya mazishi inafanyika ila bado haijajulikana kama atazikwa Dar ama kwao Kilwa. Habari tutaoa kadri ziavyoingia. Mtaa Kwa Mtaa Blog inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wa taarabu kwa kuondokewa na kipenzi chao Nasma Khamisi Kidogo.na Mungu amlaze mahala pema Peponi Mama Yetu Nasma Khamis Kidogo.


Amein

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad