HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 18, 2009

WISDOM NETWORK FILM PRODUCTION: vijana wanakuja kwa kasi katika nyanja ya filamu

baadhi ya wasanii wa WISDOM NETWORK wakiwa katika moja ya mazoezi yao ya kuigiza,ndani ya ukumbi wa disko wa Swiss pub jana jioni.
mwalimu wa kundi hilo (mwenye tai) akiigiza kama bosi aliekasirika pindi mfanyakazi wake alipoharibu kazi aliyopewa na bosi wake huyo.
wadada hawa nao waliigiza kama walivyoigiza waliopita.
hapa ni kundi zima la WISDOM NETWORK FILM PRODUCTION,wakiwa katika picha ya pamoja.wadau tunapaswa kujitoa kwa hali na mali ili kuwafanikisha vijana hawa kufika mahala wanapotakiwa kufika.hapo chini kuna historia yao fupi,naomba muipitie kwa makini ili kujua ni kitu gani wakifanyacho na malengo yao.


HISTORIA FUPI YA WISDOM NETWORK FILM PRODUCTION

WISDOM NETWORK:
maana yake ni mtandao wa Hekima,Mtandao huu unajishughulisha na sanaa ya uigizaji wa filamu,ambao umekusanya wasanii toka sehemu mbalimbali na kuungana kwa pamoja ili kukuza vipaji vyetu vya sanaa ya uingizaji wa Filamu hapa Nchini.

MWANZO WA NETWORK:
mtandao huu ulianza rasmi November 23,2008 na Mwanzilishi wake akiwa ni Ndugu Steven Mwalukasa ambaye hadi sasa ni kiongozi wa mtandao huu.

SABABU ZA KUANZISHA MTANDAO

a.Kusaidia wasanii wadogo wadogo na kuinua vipaji vya wale wanaoanza kuingia katika nyanja hii ya uigizaji (Underground) ili kuweza kufikisha mbali kiusanii

b.Kuwasaidia wasanii kupata mambo ambayo huwa wanayakosa kuyapata kutoka sehemu wamazotokea kisanaa,mambo hayo ni :

i) Ushauri wa namna ya kuishi maisha safi wakiwa katika maisha ya kawaida ya sanaa kwenye jamii.

ii) Kuwasaidia wasanii mbinu mbalimbali za kuepukana na utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na kupambana na magonjwa yatokanayo na maambukizi ya aina yeyote ile.

iii) Kuwafahamisha wasanii kwamba kwa kupitia Elimu hiyo ndogo wanayopata kutoka katika mtandao huu,kisaikolojia inamjengea moja ya silaha ya kuweza kupambana na maisha duni na kumfanya aweze kuwa na maisha bora na yaliyo marefu,pia kumfanya aheshimike na kila mtu katika jamii inayomzunguka.

iv) Kwa kupitia filamu zetu,tunaweza kufikisha ujumbe katika jamii inayotuzinguka kupitia sanaa yetu,pia kutuwezesha kujiinua kiuchumi kutoka katika hali duni na kutuwezesha kuwa na maisha yaliyobora.

MALENGO:
Tangu tulipoanza na mpaka kufikia tulipo sasa,tumekuwa tukijiwezesha wenyewe kama wana mtandao,hivyo kutokana na hali hiyo inatubidi tujitoe kwenu wanajamii ili kutuwezesha kupata udhamini ambao utatuwezesha kiutendaji,ili tuweze kutimiza malengo yetu ya kutengeneza Filamu bora hapa Nchini na nje ya Nchi yetu.

(b) Kupata ofisi maalumu ya kutufanya tuweze kukutana tunapohitajiana.

(c) Kupata Sare za mtandao,kama vile t-shirt zenye nembo ya WISDOM NETWORK

(D) Kusaidia watu wasiojiweza na kutembelea vituo vya watoto yatima (haya yote yatafanyika iwapo tutafanikiwa kukua kiuchumi.

Mwisho wa historia fupi,Ahsante kwa kushiriki kusoma waraka huu.


WISDOM NETWORK IS POWER AND FAITHFULLNESS
0754 700 639 – 0715 700 639
Stevar8rover@yahoo.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad