Kocha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Marcio Maximo(Pichani) ameongezwa mkataba na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya kuridhika na kazi aliyoanza kuifanya ambayo imeipandisha chati Tanzania katika medani ya soka.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema hayo Juni 18 jijini Dar es Salaam mwezi mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema hayo Juni 18 jijini Dar es Salaam mwezi mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili.
Mkataba wa miaka miwili aliosaini kocha huyo kutoka Brazil utamalizika mapema mwezi ujao.“ Maximo aliingia mkataba nasi wa miaka miwili kuanzia Julai 28,2006 hivyo mkataba wake huo utakamilika Julai 2,mwaka huu hivyo tumeona ni vema tulizungumzie jambo hili mapema na tumeamua kumwongezea mkataba huo kwa miaka miwili mingine” alisema Tenga.
Hatahivyo Tenga alisema pamoja na TFF kuamua kumwongeza mkataba wa kwa miaka miwili mingine na Kocha Maximo katika mazungumzo yao juu ya kuongezwa mkataba huo ameomba uongezewe mwaka mmoja tu kutokana na sababu zake binafsi ambazo hakuzitaja.
Akizungumza mara baada ya Tenga kutangaza uamuzi wa TFF kumwongezea mkataba wa kuinoa Stars, Maximo alisema sababu kubwa ya kufurahia jambo hilo na kushukuru kwa ushirikiano aliopewa kutekeleza majukumu yake na kueleza kuwa sababu yake ya kuomba apewe mwaka mmoja tu katika mkataba mpya ni kutoa nafasi kwa makocha wengine kuendeleza pale alipofikia katika programu ya kuinua na kuendeleza soka la Tanzania.
“ Unajua mtu huwezi kutekeleza programu ya miaka 10 ya kuinua na kuendeleza soka la nchi pekee yako kwani kila programu ya kocha ina muda wake wa kukamilika hivyo katika mikaka hiyo 10 kuna ulazima wa kocha mwingine kuja kuendeleza pale nilipofikia” alisema Maximo
No comments:
Post a Comment