MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amewaongoza Mawakili wa Serikali kutoa huduma za ushauri wa Kisheria kwa wananchi wakati wa Kliniki ya Sheria bila malipo iliyozinduliwa tarehe 16 Februari, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Johari amemuhudumia mwananchi aliyekuja kupata huduma ya ushauri wa kisheria ambapo alimsikiliza na kumuhudumia Sarah Mohamed aliyewasilisha malalamiko yake kuhusiana changamoto ya mirathi inayomkabili.
“Tumeyapokea malalamiko yako na mimi pamoja na timu tutayafanyia kazi kwa haraka ili kuweza kutatua changamoto inayokukabili”. Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Katika zoezi hilo la kutoa huduma kwa wananchi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Zainab Katimba.
Timu ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepiga kambi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutoa huduma mbalimbali za kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 hadi 22 Februari, 2026.




.jpeg)
No comments:
Post a Comment