Mbunge wa jimbo la Kibamba,Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki ameshiriki Baraza la Wazazi Wilaya ya Ubungo kama Mgeni Rasmi, ambapo amewashukuru wajumbe wa jumuiya hiyo kwa mchango wao mkubwa katika kukipambania Chama Cha Mapinduzi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Kairuki aliwapongeza wazazi kwa ushindi mkubwa wa asilimia 97% waliompatia Samia Suluhu Hassan, na kuwasilisha salamu nyingi kutoka kwake kwenda kwa Jumuiya hiyo. Alieleza kuwa ushindi huo ni ishara ya mshikamano, uaminifu na juhudi za pamoja katika kuimarisha Chama na Taifa kwa ujumla.
Aidha, aliwakumbusha wazazi wajibu wao wa kuendelea kuwa walezi bora kwa vijana. Alisisitiza umuhimu wa wazazi kukaa na watoto wao, kuwalea katika maadili mema, na kuwaandaa kuwa viongozi bora wa kesho watakaolisukuma mbele Taifa.
Katika mkutano huo, Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo iliwasilisha changamoto ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa jumuiya hiyo (Katibu wa Wazazi Wilaya), wakieleza kuwa ukosefu wa makazi rasmi unakwamisha utendaji kazi wa kila siku. Baada ya kupokea ombi hilo, Mheshimiwa Kairuki aliguswa na changamoto hiyo na kuahidi kuchangia shilingi milioni kumi (10,000,000) kama mwanzo wa ujenzi wa nyumba hiyo.
Pia aliwapongeza kwa uwekezaji wao wa kujenga Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ubungo, akiahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuimarisha jumuiya hiyo na kuendeleza maendeleo ya Wilaya.


.jpeg)

No comments:
Post a Comment