HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 3, 2025

FCC YAKUTANA NA MAMLAKA ZA UDHIBITI KISEKTA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHINDANI DUNIANI

📍 Dar es Salaam 

 Tume ya Ushindani (FCC) imefanya semina kwa Mamlaka za Udhibiti Kisekta kujadiliana juu ya masuala ya ushindani kwenye soko.  

Akizungumza  katika semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa FCC Bi. Khadija Ngasongwa  amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kujadili utekelezaji wa majukumu ya FCC yanayoingiliana na Taasisi hizo za Serikali ili kuhakikisha ushindani unashamiri katika mnyororo wa shughuli za kiuchumi na kumlinda mlaji.  

Amesema kuwa hivi karibuni uwekezaji umeongezeka sambamba na maendeleo ya Teknolojia pamoja na mabadiliko ya mifumo ya biashara ambayo yameleta fursa nchini lakini yameibua changamoto mpya katika kudhibiti masoko.
Ngasongwa amesema kuwa kuwa katika mabadiliko na fursa zilizojitokeza katika soko  kunahitaji maarifa na mbinu na uelewa wa kisasa na bila kufanya hivyo tutaachwa nyuma na kushindwa kulinda maslahi ya watumiaji na wawekezaji kwa usawa.

Aidha amesema semina hiyo itajenga uelewa wa pamoja juu kanuni za ushindani na dhima ya kila mdhibiti wa kisekta katika kuhakikisha masoko yanafanya kazi ipasavyo,kukuza ushirikiano  kati ya FCC na Wadhibiti wa Kisekta ili kuweza kubadilisha taarifa ,uzoefu na mikakati ya pamoja.

Ameongeza kuwa hii ni fursa kwa Wadhibiti wa Kisekta kukutana na kujadili changamoto zilizopo katika mazingira ya biashara pamoja na kujengeana uwezo kwa wataalamu wetu ili wawe na ujuzi wa kukabiliana na vitendo vya kandamizi na hadaifu sokoni. 

Aidha, FCC itahakikisha kuwa ushindani nchini unaendeshwa kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na taratibu na haziwezi kutekelezwa na Tume peke yake bila ya uwepo wa wadhibiti wa kisekta kama ambavyo imebainishwa kwenye sheria zinazotusimamia. 

Sekta tunazozisimamia zina mchango na uhusiano wa karibu na maslahi ya wananchi hivyo changamoto katika sekta moja zinaweza kuathiri wananchi na Ustawi wa Taifa. 

Kilele cha Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu ya "Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani" ambayo itafanyika Desemba 5, 2025 katika Hoteli ya King Jada, Jijini Dar es Salaam. 

Semina hiyo imefanyika Desemba 03, 2025 katika Ofisi za FCC, Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Khadija Ngasongwa  akizungumza wakati akifungua mkutano wa kujengeana uwezo na  Wadhibiti wa Kisekta,jijjni Dar es Salaam.

Baadhi ya Matukio katika Semina ya kujengeana uwezo Wadhibiti wa Kisekta kuelekea Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani Desemba 5 ,2025 jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Khadija Ngasongwa akiwa katika picha ya pamoja na Wadhibiti wa Kisekta katika kuelekea Kilele cha  maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani yatayofanyika Desemba 5 ,2025 jijini Dar es Salaam.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad