Serikali imeandaa mkakati maalumu wa kutambua mahitaji ya teknolojia nchini (Technology Road Map) kwa kipindi cha miaka 20 hadi 30 ijayo, ili kuhakikisha teknolojia zinazofundishwa katika taasisi za elimu zinajibu mahitaji halisi ya wananchi na kuchochea maendeleo ya taifa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Ladislaus Anyoni, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi bora wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
Prof. Anyoni amesema kuwa ili taifa lipige hatua, wataalamu hawapaswi kuridhika na elimu wanayoipata chuoni pekee, bali wanapaswa kujikita katika vituo vya umahiri vilivyopo nchini kwa lengo la kuendeleza ujuzi na ubunifu. “Kwa sasa nchi nzima tunavyo vituo 10 vya umahiri, ambavyo vina jukumu la kukuza ubunifu na kuongeza ujuzi katika taaluma mbalimbali,” amesema.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwekeza zaidi katika teknolojia ili kupunguza utegemezi wa vifaa kutoka nje ya nchi, hatua itakayosaidia kukuza uchumi na kuongeza uwezo wa nchi kujitosheleza katika uzalishaji wa vifaa vya kiteknolojia.
“Tunatamani tufike hatua kama nchi nyingine ambapo sisi wenyewe tutakuwa watumiaji wa teknolojia tunazozalisha. Tukifika huko, mapinduzi ya viwanda yatakwenda kwa kasi zaidi kwa sababu yataakisi mahitaji halisi ya jamii,” amesema.
Ameishukuru pia taasisi na wadau waliotoa tuzo na zawadi kwa wanafunzi, akisema hatua hiyo inachochea hamasa kwa vijana kupenda masomo ya sayansi na kuendeleza ubunifu nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Preksedis Ndomba, amewataka wahitimu kutobweteka na shahada walizopata, bali wajikite katika ujasiriamali na kutoa huduma za kitaalamu wanazoweza kuzalisha kutokana na ujuzi walioupata chuoni.
“Hakuna tatizo la fedha; tatizo ni namna tunavyoweza kuuza talanta na ubunifu tulionao. Ufaulu ni muhimu, lakini hatutakiwi kuutangaza zaidi ya kutangaza ubunifu na huduma tunazoweza kutoa,” amesema Ndomba.

No comments:
Post a Comment