WANANCHI wamehaidi kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 Oktoba 2025 siku ya uchaguzi Mkuu kupiga kura ya Rais, Mbunge na Diwani kwa kishindo.
Wananchi hao ambao ni wakazi wa Kata ya Lukuledi wametoa ahadi hiyo sio tu kwamba ni haki yao kikatiba bali wameona kazi kubwa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ilivyo tendewa haki kivitendo.
"Sisi bila hata kutuambia ni lazima tutaenda kutiki tu, kupiga kura maana kazi nzuri tunaiona na sisi akina Mama, Vijana na Walemavu tunaona namna mikopo ya asilmia 10 ilivyo tukomboa kiuchumi. Tumepata fedha nyingi za mikopo awamu hii ya Rais Samia kuliko awali." alisema Rehema Mohamed mkazi wa Kijiji cha Lukuledi.
Hayo yamejili kwenye ziara ya Afisa Tarafa Emmanuel Shilatu ya kutembelea na kujionea maendeleo ya vikundi vilivyo pata mikopo hiyo ambapo pia Gavana Shilatu alitumia Wasaa huo kuwasisitiza Wananchi hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi.
"Nawapongeza wote wanufaika wa mikopo iliyotolewa na Serikali iliyopo Madarakani na mnakiri ukubwa wa mikopo na ukubwa wa ukombozi kiuchumi mlioupata. Lakini kubwa zaidi nawasisitiza pia kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu. Serikali tumejipanga vilivyo kuhakikisha zoezi hilo halali kwa mujibu wa katiba linafanikiwa." Alisema Gavana Shilatu
Kwenye ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata na Afisa Maendeleo kata. 29 Oktoba 2025 Wananchi kote nchini wenye sifa watashiriki zoezi la kupiga kura kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.
No comments:
Post a Comment