HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 20, 2025

FARU WEUSI 8 ULINGONI LEO UBINGWA WA AFRIKA KANDA YA 3 NAIROBI


▫Wakongwe Mbonabucha, Mbundwike na Ezra kuwaongoza vijana wanaochupikia

Okoba 20,2025, Nairobi - Kenya.
Mabondia 8 wa Kikosi cha timu ya ngumi ya Tanzania almaarufu kama "FARU WEUSI" watapanda ulingoni leo Jijini Nairobi, Kenya katika mashindano ya Afrika Kanda ya 3 Nairobi 2025.

Wachezaji hao wataongozwa na Wakongwe Kassim Mbundwike, mshindi wa medali ya Shaba Jumuiya ya Madola Birmingham 2022 atakayepambana na Mazongo Anderson kutoka DR Congo katika uzani wa Light middleweight 71kg huku George Mbonabucha dhidi ya Kumbo Mwinyi kutoka Kenya B na Ezra Paul akipimana ubavu na Washington Wandera kutoka Kenya A.

Jumla ya mapambao 32 yatapiganwa leo katika Uwanja wa ndani wa Kasarani katika sessions mbili za mchana (Saa 8 kamili) na jioni (Saa 12)

Ratiba kamili ni kama ifuatavyo:-
Mchana
Light fly 48 kg
1. Juma Athumani vs Abednego Kyalo (Kenya A)

Light weight 60 kg
2. Ezra Paulo vs Washington Wandera (Kenya B)

Welterweight 67 kg

3. Shafii Mbaraka vs Lendoye Arthur (Gabon)
Jioni

Fly weight 51 kg

4. Aziz Chala vs Tulembekwa Zola (DR Congo)

Featherweight 57 kg

5. George Mbonabucha vs Kumbo Mwinyi (Kenya B)

Light welterweight 63.5 kg

6. King Lucas vs Engo Mba Laurent (Gabon)

Light middleweight 71kg

7. Kassim Mbundwike vs Manzongo Anderson

Heavyweight 92 kg


8. Emmanuel Augostino vs Abdoul Ringo (Uganda)
Ratiba kamili ya leo imeambatanishwa.

✍🏽 Mawasiliano BF

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad