Hifadhi ya taifa ya Kisiwa cha Rubondo yenye Kilomita 150 wa mzunguko wa fukwe ndiyo chanzo kikuu cha mazalia ya samaki kutokana na kuwepo kwa maeneo ya kustawisha uoto kwenye fukwe ambapo ndiyo mazingira rafiki kwa mazalia ya samaki.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Imani Kikoti amesema kutokana na uhaba wa samaki sehemu zingine katika ziwa hilo imepelekea kupambana na majangili ambao wanafanya uvuvi haramu katika eneo la hifadhi hiyo.
"eneo letu la hifadhi inanufaisha wakazi Milioni 4.5 kutokana na uoto wa asili kwenye fukwe zetu ambapo samaki wakiwa wengi upande wetu hua wanatoka na kusambaa maeneo mengine hasa vijiji zinazozunguka hifadhi yetu na kunufaika na mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo" amesema Dkt. Kikoti
Hifadhi kwa sasa imeanza program ya kuwahamasisha vijiji zinazozunguka hifadhi hiyo kujenga vizimba na kutenga maeneo ambayo yatawezesha kustawishwa kuwa na uoto wa kwenye fukwe kwa ajili ya mazalia ili kuongeza wingi wa upatikanaji wa samaki maeneo yao na kupunguza wavuvi haramu katika hifadhi hiyo ambao wanavamia kwa kukosa samaki maeneo yao.
Hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo upande wa ardhi ina ukubwa wa Kilomita za mraba 237 na eneo la maji Kilomita za mraba 220 na kuwa na ujumla wa ukubwa kilomita za mraba 457.Baadhi ya wakazi wa vijiji zinazozunguka hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo wamesema kwa sasa wanapata samaki wengi ambao wengi wao wanatoka katika hifadhi ya kufika maeneo ya vijiji vyao kutokana na kuzaliana kwa wingi maeneo ya hifadhi na imewasaidia kukua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment