HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 1, 2025

ZIMBABWE YATAMBUA MCHANGO WA TANZANIA UKOMBOZI WA NCHI KUSINI MWA AFRIKA

 



*Zimbabwe yaiheshimu Tanzania kwa mchango wake katika ukombozi wa Kusini mwa Afrika

SERIKALI ya Zimbabwe leo imetoa heshima na shukrani kwa Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika kuzikomboa nchi za Kusini mwa Afrika.

Akizungumza Kaole – Bagamoyo leo Agosti 31, 2025 Makamu wa Pili wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi, alitoa shukrani hizo kufuatia Tanzania kusimamia mapambano ya ukombozi,kwa kuwapa hifadhi, na maeneo waliyoyatumia kuwanoa wapiganaji wao walioikomboa nchi yao ya Zimbabwe na kwamba bila ukarimu wa Tanzania mapambano yao yasingefanikiwa.

Mohadi pia alimpongeza shujaa wa Afrika, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyesimama kidete kuhakikisha ukombozi hauwi tu kwa Tanzania wa pekee bali wa bara zima la Afrika.

Aidha, alisisitiza kuwa mshikamano kwa viongozi na mataifa ya Afrika unapaswa kuimarishwa ili kuiinasua katika hali ya uchumi.

“Afrika imepata uhuru wa kisiasa, lakini mapambano ya uhuru wa kiuchumi bado yanaendelea. Tukiwa wamoja, tutayashinda,” alisema.

Kaole - Bagamoyo imetajwa kuwa sehemu iliyowahi kuwahifadhi viongozi mashuhuri wa ukombozi kama Samora Machel, Joaquim Chissano na Emmerson Mnangagwa.

Mohadi alihitimisha salaam zake kwa kutoa wito kwa vijana wa Afrika akis3ma“Dumisheni mshikamano, uzalendo na kujitolea ili kuhakikisha dira ya Afrika huru na yenye mshikamano inatimia kikamilifu.”

Ujumbe huo wa Zimbabwe umekamilisha ziara ya siku mbili Mkoani Pwani ambapo Mkuu wa Mkoa huo Abubakar Kunenge jana aliwatembeza kwenye shule ya uongozi ya Mwl. Julius Nyerere Kibaha kwa - Mfipa na leo wenye kumbukumbu ya makazi ya wanaharakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika yaliyopo Kaole - Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Zimbabwe na Tanzania, sambamba na kuheshimu historia ya pamoja ya harakati za ukombozi barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad