HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 4, 2025

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 100 ZATOLEWA NA MGODI WA BARRICK KWA MWAKA 2025 - CSR

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale kwa mwaka 2025 imepokea kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Barrick kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vinne (4) vya Madarasa kupitia mpango wa Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR). 
Mradi huo umetekelezwa kwa mfumo wa Force Account ambapo kwa mujibu wa Mkataba, mradi ulianza tarehe 30/04/2025 na unategemewa kukamilika tarehe 11/09/2025 huku mpaka sasa ukifikia 85%.
Mwenge wa Uhuru 2025 umekagua na kuridhia mradi huo na kuweka jiwe la msingi,  na utakapokamilika utapunguza mlundikano wa wanafunzi na kupunguza tatizo la upungufu wa madarasa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad