Mradi wa Maji wa Visima vitano vya Jimbo unatekelezwa katika Vijiji vitano ambavyo ni Kanegele, Mwingiro, Shabaka, Wavu na Lubando vilivyopo Halmashauri ya wilaya ya NYANG’HWALE Mkoani GEITA.
Mradi huu vyanzo vyake ni visima virefu (05) vyenye uwezo wa kutoa Maji jumla ya lita 21,150 kwa saa na kina tofauti tofauti. Mkataba wa ujenzi wa Vioski ulianza rasmi mnamo tarehe 06/01/2025 na unatarajiwa kukamilika 30/09/2025. Mradi unatekelezwa kwa Force Account na Local Fundi Taragwa T. Taragwa.Gharama za utekelezaji Mradi wa maji katika Vijiji hivi vitano (5) ni shilingi 327,099,202.00. Hadi sasa Jumla ya kiasi cha shilingi 137,150,818.50 kimekwisha lipwa kwa ajili ya shughuli ya ufungaji wa Sola, pampu, ununuzi wa matenki na malipo ya Local Fundi. Chanzo cha fedha za Mradi huu ni kupitia Mpango wa Malipo kulingana na Matokeo (PforR) na Fedha Maalum (Special Fund). Kazi zilizokwisha tekelezwa hadi sasa ni Ufungaji wa mfumo wa sola na pampu, Ujenzi wa Vioski, kuweka mfumo wa maji na tenki la plastiki lenye ujazo wa lita 10,000, Uchimbaji na ufukiaji wa mitaro ya bomba yenye urefu wa mita 9,467. Kazi ambazo bado hazijatekelezwa ni ukamilishaji kwenye vioski, ujenzi wa chemba na fensi. Mara baada ya Mradi kukamilika utaendeshwa na CBWSOs ya Nyamtukuza. Utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 85.\Faida za Mradi huu ni kama ifuatavyo ;Wananchi takribani 5,000 waishio katika Vijiji hivyo watapata huduma ya maji safi na salama hivyo kupunguza magonjwa ya milipuko.
Mwenge wa Uhuru umeridhia kuweka jiwe la msingi la msingi katika mradi huo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,ISMAIL ALI USSI.
No comments:
Post a Comment