Na Khadija Kalili ,Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Frederick Faustine Komba ametoa wito kwa vijana waliohitimu mafunzo ya kwa mujibu wa sheria Operesheni Nishati Safi 2025 kutomezwa na mitandao ya kijamii kwa sababu imekua chanzo cha kupoteza maadili .
DC Rufiji Luteni Kanali Komba amesema hayo wakati alipokua mgeni rasmi kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya Oparesheni Nishati Safi katika Kikosi 830 Kibiti Mkoani Pwani.
"Zamani kulikua na sherehe za jando kwa wanaume na unyago kwa mabinti ambao walifindwa namna ya kuishi vizuri katika jamii hivyo basi mafunzo haya kwa vijana yanayotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yamebeba maudhui hayohayo ya kuwafundisha vijana namna ya kuishi vema katika jamii.
Akifunga mafunzo hayo ya Operesheni Nishati Safi Luteni Kanali Komba ametoa pongezi kwa Mkuu wa Kikosi cha Kibiti 830 Mohammed Karuma pamoja na wakufunzi wote kutokana na mafunzo waliyoyatoa kwa vijana hao.
"Natoa pongezi zangu za dhati kwa Mkuu wa Kikosi Kanali Mohammed Karuma pamoja na wakufunzi wote kwa ujumla kutokana na mafunzo waliyoyatoa kwa vijana hawa ambao wametoka katika Mikoa mbalimbali mbalimbali nchini mwetu huku wote wamekua wamoja" amesema Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Luteni Kanali Komba.
Amesema kuwa weledi wa wakufunzi hao umewabadilisha vijana hao na kuwa wamoja na kuwasisitiza wahitimu hao waende kuishi waliyofundishwa.
"Nendeni mkawe mabalozi wazuri wa mafunzo ya JKT huko muendako mkawe wawakilishi wema pia mtambue kwamba maisha siyo rahisi mkajitunze na kuwa timamu kitabia na kiafya sababu ninyi ndiyo viongozi wa taifa letu kesho" amesema DC Rufiji Luteni Kanali Komba.
Wakati huo huo amewataka vijana waliohitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT kwa Mujibu wa sheria 2025 kulinda kiapo chao na kutenda yale waliyofundishwa pindi watakaporejea nyumbani.
Yamesemwa hayo na aliyekuwa mgeni rasmi katika kufunga mafunzo kwenye sherehe iliyifanyika tarehe 18 Septemba 2025,yanayofahamika kama Operesheni Nishati safi katika kikosi 830 Kibiti kilichopo Mkoani Pwani.
Naye Mkurugenzi Rasilimali Watu Makao Makuu ya Jeshi Brigedia Jenerali Simon Pigapiga kwa Niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob Mkunda amewataka vijana wanaohitimu mafunzo hayo kutumia kwa faida ujuzi waliyo upata katika kipindi chote cha mafunzo yao.
Aidha Kanali Aranyael Nnko ambaye ni mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa kipindi cha majuma 12 yakijumuisha mafunzo ya awali ya kijeshi, Kazi za mikono na uzalishaji Mali.
Wakati huohuo ametoa shukrani kwa wazazi waliotoa fursa kwa vijana wao kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria 2025 ambayo kimsingi yanamjengea Kijana Uzalendo na Moyo wa Kupenda kazi.
"JKT ni mahali sahihi na salama hivyo jamii na wazazi msisite kuleta vijana wenu kuja kupata nafasi hii ambayo huwasaidia kuwajenga kizalendo na kuwapa mafunzo ya awali ya ulinzi na usalama pia ni haki, kwa vijana wa kitanzania katika Kufundishwa Uzalendo na siyo vinginevyo" amesema Luteni Kanali Komba.
No comments:
Post a Comment