HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 27, 2025

TARURA yajenga madaraja nafuu 453 , yaokoa Sh. Bilioni 83

Mhandisi Mshauri wa TARURA Pharies Ngeleja akuzungumza na waandishi wa habari katika banda la TARURA katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa Raise unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa TARURA Makao Makuu Ephraim Kalunde kuhusiana mradi huo unavyotekelezwa na kuleta matokeo jijini Dar es Salaam.

*Daraja la Mwanagati kujengwa kwa Sh. Bilioni 1.6, mkandarasi apatikana

Na Mwandishi Wetu
WAKALA wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA)imesema kuwa imejenga madaja nafuu na rahisi 453 kwa kwa gharama sh.bilioni 34 ambapo wangejenga kwa kutumia zenge madaraja hayo yangetumia gharama ya sh.bilioni 117.

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) uliofanyika jijini Dar es Salaam Mhandisi Mshauri wa TARURA Makao Makuu Pharies Mgeleja amesema kuwa daraja ni uchumi kutokana na kuweka mawasiliano kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na asili ya barabara kuunganisha sehemu moja lazima kuwepo kwa kwa daraja.

Amesema kuwa sasa wako katika hatua ya kujenga daraja refu la Mwanagati Magole katika Mto Mzinga, Temeke, Dar es salaam litakalojengwa kwa kutumia teknolojia ya Mawe litakalo gharimu. sh.Bilioni 1.6 na mkandarasi ameshapatikana.

Ngeleja amesema kuwa wamejenga barabara kwa kutumia mawe Kilomita 29.3 katika Mikoa ya Rukwa ,Mwanza,Kigoma pamoja na Morogoro kwa kugharimu sh.bilioni 11 huku kilomita 33 zikijengwa kwa Lami

Amesema kuwa changamoto iliyokuwa mkoani Mwanza iliyokuwa ikiwakabili wananchi ya Nata kwenda Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando walikuwa wanazunguka kilomita 10 lakini sasa imebaki Historia baada kujengwa miundombinu bora ya barabara.

Kwa upande Msimamizi Mradi wa Raise Mhandisi Ephraim Kalunde amesema kuwa Mradi Raise ni uibuaji wa fursa za kiuchumi vijijini wa ujenzi wa barabara na Matengenezo.

Amesema mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unaotekelezwa katika Wilaya za Iringa mkoani Iringa ,Handeni mkoani Tanga ,Ruangwa mkoani Lindi ,Morogoro mkoani Morogoro pamoja na Mbogwe mkoani Geita ambapo mradi huo ulianza Novemba 2021 na kumalizika Juni 2027.

Mhandisi Kalunde amesema kuwa mradi huo ni ujenzi wa Barabara kutoka kiwango cha Changarawe kwenda kiwango cha Lami

Aidha amesema eneo la lingine ni ujenzi wa vivuko ambapo hadi sasa wamejenga vivuko zaidi ya 2000 kati ya vivuko 4500 sawa na na kufanya fursa za kiuchumi kwa wananchi zaidi ya milioni mbili.

Hata hivyo amesema mradi huo wanatumia vikundi vya wananchi kwa barabara Kilomita tano katika kufanya matengenezo ya mitalo ,kuziba mashimo pamoja na kukata nyasi ikiwa ni lengo la kuwainua kiuchumi ambapo vikundi hivyo wataanza vitaanza katika Wilaya Nane za mfano katika mikoa 12.

Amesema kazi za vikundi zinarahisisha katika kufanya barabara hizo kuwa tayari muda wote kuliko kusubiri kupatikana kwa mkarandarasi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad