Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti ya Uandishi wa Habari wa Matumizi ya Umeme Jua katika Kilimo ,jijini Dar es Salaam.
Balile na Mukiza wakionesha ripoti ya utafiti kwa waandishi wa habari ,jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Utafiti wa Matumizi ya Umeme Jua katika Kilimo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma Dkt.Darius Mukiza akiwasilisha ripoti ya utafiti kwa waandishi wa habari kuhusiana Uandishi wa habari wa Matumizi ya Umeme Jua katika Kilimo
*Ripoti ya 2026 Tanzania kufanya vizuri kutokana na nguvu katika matumizi ya nishati safi
Na Mwandishi Wetu
UTAFITI huo wa ripoti ya Uandishi wa Habari wa matumizi ya Umeme Jua katika Kilimo unaonyesha Tanzania kushika nafasi ya Tatu kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo katika ripoti nyingine ya 2026 kasi itaongezeka kutokana Serikali kuweka nguvu katika matumizi ya nishati safi.
Ripoti hiyo imetolewa na Kituo cha Umahiri kwenye vyombo vya habari (African Centre for Media Excellence) ukifadhiliwa na Taasisi ya MOTT (MOTT Foundation) ikionyesha, Tanzania kushika nafasi ya tatu uandishi wa habari huku Kenya ikipata nafasi ya kwanza na Uganda ikiwa nafasi ya pili.
Uandishi wa Habari matumizi ya nishati jua kwenye kilimo waongezeka Afrika mashariki kutokana na kutolewa na mafunzo ya kuwajenge uwezo vyombo vya habari.
Utafiti huo ulifanywa 2023 ulitokana na kubaini uandishi hafifu habari hizo kwenye nchi tatu za EAC ni uelewa wa Waandishi kwenye habari hizo kuwa chini hivyo baada ya utafiti walijengewa uelewa na kuwezeswa fedha kuandika habari hizo.
Utafiti mpya umebaini nchi tatu za Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda, zimekuwa na ongezeko la uandishi wa habari za matumizi ya umeme jua katika kilimo,
Kenya imeongoza miongoni mwa nchi hizo kutoa habari 43 za matumizi ya umeme wa jua kwenye kilimo ikiwa ni asilimia 38.1,Uganda habari 36 sawa na asilimia 31.9 huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu ikiwa imechapisha habari 34 sawa na asilimia 30.1.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo Dar es Salaam Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa umma Dkt.Darius Mukiza amesema utafiti huo umefanyika kuanzia Januari Mosi hadi Desemba 2024.
Utafiti kwa upande Tanzania ulihusisha vyombo vya habari vya Mwananchi Communicationi Limited (MCL) pamoja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ,Kenya vyombo vya habari vilivyotumika ni gazeti la Daily Nation,Shirika la Taifa la Utangazaji (KBC) na upande wa Uganda, ni Shirika la Taifa la Utangazaji (UBC) na gazeti la New Vision.
"Taarifa za matumizi ya umeme wa jua kwenye kilimo zimeongezeka kwa asilimia 79 kutoka habari 63 mwaka 2023 hadi 113 mwaka 2024, pamoja na ongezeko hilo uandishi umeegemea zaidi habari za matukio yaliyohusisha Serikali, mashirika binafsi.
Dkt.Mukiza amesema Habari za uchunguzi na zilizofanyiwa tathmini ya kina hazikuonekana kwenye vyombo hivyo wakati utafiti ukifanyika.
Gazeti la mwananchi limetumika kwenye utafiti huo, liliachapisha habari kwa asilimia 52.9 ikifuafiwa na TBC kwa asilimia 47.1.
Dkt.Mukiza amesema jambo lingine walilobaini wakati wa utafiti huo,habari za matumizi ya nishati jua kwenye kilimo hazikuonekana kama habari za kuvutia wateja hivyo hazikupata nafasi za mwanzo ndani ya vyombo vya habari.
"Pia habari zilizochapishwa hazikuzingatia usawa wa kijinsia, asilimia 72.2 ya habari zilimnukuu zaidi ya mtu mmoja mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo ni asilimia 32 pekee, sauti za wanaume zilikuwa asilimia 74,Kenya wanawake wamehusishwa mara nyingi kwenye habari ikilinganishwa na Uganda na Tanzania"amesema.
Akizindua utafiti huo,Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEC) Deodatus Balile amesema habari za matumizi ya umeme wa jua kwenye kilimo zinahusisha kwenye umwagiliaji,ukaushaji wa mazao kwa lengo la kusafirisha nje ya nchi ikiwa yameingezewa thamani na kuachana matumizi ya kuni.
Amesema licha ya kuonekana kwa ongezeko hilo habari za uchunguzi bado ni changamoto upatikanaji wake ambapo jitihada zinahitajika kwa waandishi wa habari katika matumizi ya umeme jua katika kilimo.
Amesema matumzi ya ya umme jua katika kwenye kilimo zipo faida apatazo mtumiaji kulingana na wataalamu mbalimbali ikiwamo kukausha viungo kwa asilimia 70 kwa kila kirutubisho kwenye mazao, kwa sababu hairuhusu kupenya kwa mionzi ya jua.
Pia umeme Jua hairuhusu mionzi ya jua ukianika karafuu na mdarasini, ukianika juani inaondoa uhalisia hata kibiashara inakuwa ngumu.
Picha ya pamoja ya waandishi wa habari walioshiriki uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Uandishi wa Matumizi ya Umeme Jua katika Kilimo,jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment