Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hiyo aina ya Toyota Hilux Jijini Dodoma, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo amesema kuwa uwepo wa gari hiyoutasaidia utekelezaji wa majukumu ya kila siku hatua itakayosaidia kuongeza tija, ufanisi na kuleta matokeo chanya yatakayosaidia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikalimkoani Manyara kufikia malengo iliyojiwekea kwa wakati.
Aliongeza kuwa uwepo wa gari hiyo ni jitihada za Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuuwa Serikali kuboresha mazingira ya utendaji kazi hasa ukizingatia jiografia ya Mkoa huoambapo Mawakili wamekuwa wakitumia muda mrefu kutoa huduma kutokana na umbaliuliopo kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine.
Kwa upande wake Wakili Mfawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa waManyara ndugu Lameck Butuntu ameishukuru Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwakuwapatia gari hiyo huku akifafanua kuwa gari hiyo itasaidia kupunguza changamoto zakiutendaji zilizokuwepo kwa kuwa sasa wataweza kutekeleza majukumu yao kwa wakatiikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo ikiwemo yalemaeneo yaliyokuwa hayafikiki kwa wakati.
Alieleza kuwa, ujio wa gari hiyo utasaidia kutembelea wilaya, tarafa, Kata za mkoa huokwa wakati ili kuhakikisha wanaisaidia Serikali na wananchi kupata haki kwakutembelea maeneo yenye migogoro hatua itakayosaidia kuendesha na kumalizamashauri hayo kwa wakati.
Aidha, Ndugu Butuntu alisema kuwa Mawakili wa Serikali mkoani humo sasa watafikamahakamani kwa wakati tofauti na awali ambapo iliwalazimu kuazima magari kutokataasisi nyingine za Serikali.
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mkoani Manyara, inahudumia jumla ya Wilaya tano zaMkoa huo ambazo ni Wilaya ya Babati, Mbulu, Hanang’i, Kiteto na Simanjiro.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi garikwa Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkoa wa Manyarandugu Lameck Butuntu katika makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dodoma.Anayeshuhudia kushoto ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Manyara Ndugu. Lameck Butuntu.


Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akikabidhi funguo ya gari kwa Wakili waSerikali Mfawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkoa wa Manyara ndugu LameckButuntu katika makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenyepicha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyaramara baada ya kukabidhi gari hiyo Jijini Dodoma. Wa Pili kushoto ni Mkurugenzi waIdara ya Madai ndugu Mark Mulwambo na kwanza kushoto ni Afisa Rasilimali Watu waOfisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Neema Baltazary.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akipeana mkono na Wakili wa SerikaliMfawidhi Mkoa wa Manyara mara baada ya kukabidhi gari hiyo Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment