HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 18, 2025

USAJILI WA WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA KUIMARISHA HUDUMA ZA BIMA


Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, akizungumza kwenye kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17, 2025 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna, Dodoma..

Wadau wa zao la tumbaku nchini wamekutana jijini Dodoma na kuweka mkakati wa kuhakikisha wakulima wanapata bima ya zao hilo kupitia vyama vyao vya ushirika, hatua inayolenga kuwalinda dhidi ya majanga na hasara zinazoweza kuathiri uzalishaji.

Kikao hicho kiliwahusisha Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Konsotia ya Bima za Kilimo (TAIC), taasisi za kifedha na wakuu wa wilaya za mkoa wa Tabora.

Akizungumza katika kikao hicho jana Septemba 17, 2025, jijini Dodoma, Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, alisema hatua hiyo ni mwanzo wa kuhakikisha kila mkulima wa tumbaku anakuwa na bima ya mazao kabla ya kuanza msimu mpya wa kilimo.

“Usajili wa wakulima utaanza mara moja na takwimu zitakusanywa kwa manufaa ya wakulima, taasisi za kifedha na kampuni za bima. Tunataka mfumo wa bima uwe na tija na kulinda kipato cha mkulima,” alisema Dkt. Ndiege.

Aliongeza kuwa bima kwa wakulima kwa sasa ni jambo la lazima, kwani inawalinda wanapokumbwa na majanga, huku akisisitiza kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kila mkulima wa tumbaku anakuwa na bima ya mazao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamis Mkanachi, alisema usajili na bima kwa wakulima ni hatua ya kudhibiti mianya ya utoroshaji wa tumbaku na kuhakikisha wakulima wanapata maslahi kupitia vyama vyao vya ushirika.

“Kukamilika kwa usajili kutasaidia kudhibiti vitendo vya utoroshaji, kwa kuwa mkulima atakayekopeshwa kupitia chama cha ushirika atalazimika kuuza tumbaku yake kupitia chama hicho na si vinginevyo,” alisema Dkt. Mkanachi.

Wadau hao walisisitiza kuwa bima ya mazao ni nguzo muhimu ya kulinda ustawi wa wakulima na kuongeza tija ya kilimo, jambo litakalosaidia sekta ya tumbaku kuchangia zaidi katika pato la taifa.


Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,akizungumza kwenye kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.


Kamishna wa Bima Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) - Dkt. Baghayo Saqware,akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamis Mkanachi,akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt Gerald Mongella,akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

 

Wadau mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17, 2025 jijini Dodoma.

 

Wadau mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,(hayupo pichani) wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17, 2025 jijini Dodoma.
 
Wadau mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,(hayupo pichani) wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.
  

Wadau mbalimbali wakisikiliza hotuba ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege,(hayupo pichani) wakati wa kikao cha wadau wa Tumbaku kwa ajili ya kupitisha utaratibu wa utekelezaji na utoaji wa Bima ya Zao la Tumbaku kwa wakulima kupitia Ushirika kilichofanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad