Ikiwa ni siku ya tano tangu kuwasili kwa mwenge wa uhuru mkoani Geita katika wilaya ya Bukombe mwenge umezindua vyumba 8 vya madarasa pamoja na vyoo matundu 10 katika shule ya msingi businda ambapo mradi huu umegharimu takribani shilingi milioni 222 ambapo unawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora na salama.
Akizindua mradi huo kiongozi wa mbio za mwenge Ismail Ali Ussi amesema kuwa serikali imejipanga kuboresha sekta ya elimu kwa kuwekeza nguvu kubwa katika sekta hii ili kuboresha elimu nchini.
Aliongeza kuwa kupitia miundombinu bora inayojengwa na serikali itawafanya wanafunzi wa Businda kusoma katika mazingira bora na kupandisha ufaulu katika wilaya ya Bukombe.
No comments:
Post a Comment