HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 25, 2025

MSHINDI WA ZIGO LA MWEZI LA PIKU AKABIDHIWA PIKIPIKI



Na Mwandishi Wetu
JUKWAA la kidijitali la PIKU Afrika, linaloendesha minada ya kipekee kupitia mtandaoni, leo Septemba 25, 2025 limetangaza na kukabidhi zawadi kwa washindi wa awamu ya tano ya promosheni yake ya minada ya kidijitali.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Mabibo jijini Dar es Salaam, mshindi wa kwanza Adam Ahmed Adam alikabidhiwa pikipiki mpya aina ya TVS, ikiwa imekamilika kwa bima ya chombo na bima binafsi kwa mwaka mzima, pamoja na ofa ya mafuta lita 12 kutoka kampuni ya Car Cargo General na lita 30 kila mwezi kwa mwaka mzima.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda, alisema kampuni hiyo ina lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia minada ya kidijitali.

 “Kama leo tunavyomkabidhi mshindi wetu pikipiki mpya yenye ofa ya mafuta lita 30 kila mwezi kwa mwaka mzima, hii ni fahari kubwa kwetu. Tunachofanya ni kumpa mtaji wa kuanzia kijana Mtanzania katika safari zake za kila siku,” alisema Mbunda.
Mbali na mshindi wa kwanza, mshindi wa pili alijinyakulia televisheni janja ya inchi 55 kutoka LG pamoja na rauta yenye kifurushi cha intaneti cha mwaka mzima. Mshindi huyo alieleza furaha yake akibainisha kuwa ushindi huo utamrahisishia maisha baada ya muda mrefu kuishi na rafiki yake.
Mshindi wa tatu, Jakson Ngoji, alijishindia simu janja, kifurushi cha intaneti cha mwaka mzima na spika ya Bluetooth. Alipongeza PIKU Afrika kwa uaminifu wao na kwa kuhakikisha zawadi zinakabidhiwa kwa washindi bila kuchelewa.

Kwa upande wake, Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya, alisema bodi ipo kuhakikisha kuwa michezo yote ya bahati nasibu inafuata taratibu na kanuni zilizowekwa.

 “Bodi ipo kuhakikisha kila mshiriki anashinda kwa haki bila upendeleo wowote, na zawadi zinakabidhiwa kwa mujibu wa ushindi wao. Pia tunawahimiza waendeshaji wote wa michezo ya kubahatisha kujisajili ili kuchangia pato la taifa,” alisema Mtafya.

Naye msambazaji wa pikipiki za TVS, Husein Ally, alisema kampuni yao inajivunia kushirikiana na PIKU Afrika huku akitangaza ofa ya bima ya mwendeshaji yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa mshindi.
Ili kushiriki katika minada ya PIKU Afrika, washiriki wanatakiwa kupakua App ya PIKU kupitia Play Store au Apple Store na kufuata maelekezo. Tiketi zimewekwa kwa viwango rafiki: tiketi 10 kwa Sh. 1,000, tiketi 50 kwa Sh. 5,000, tiketi 100 kwa Sh. 10,000 na tiketi 1,000 kwa Sh. 100,000.

Mbunda aliongeza kuwa minada mikubwa bado inaendelea, ikiwemo gari aina ya Toyota Raum na dhahabu, akiwataka Watanzania kuendelea kushiriki.

Kwa mara nyingine, PIKU Afrika imeonesha kuwa kinara katika mapinduzi ya minada ya mtandaoni nchini, ikiwapa wananchi fursa ya kushinda bidhaa bora kwa bei nafuu kupitia mfumo wa kidijitali, wa kipekee na wa uwazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad