HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 25, 2025

TBS Yaendelea Kutoa Elimu ya Viwango vya Madini Geita

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya madini kuhusu umuhimu wa kuzingatia viwango vya ubora, katika Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.

Akizungumza katika Maonesho hayo leo Septemba 25, 2025, Meneja wa TBS, Kanda ya Ziwa Magharibi Bw. Joseph Makene amesema shirika hilo limejikita katika uandaaji na uratibu wa viwango, ikiwemo vile vinavyohusu madini, ili kuhakikisha kuwa rasilimali hiyo muhimu inakuwa na thamani zaidi sokoni.

“TBS inatoa elimu kwa wadau wote wa sekta ya madini kuhusu viwango vya ubora ili kuongeza thamani ya madini na kuwawezesha kujiongezea kipato,” amesema Bw. Makene.

Ameongeza kuwa shirika hilo linaendelea na ujenzi wa jengo jipya la maabara mkoani Mwanza, ambapo moja ya huduma zitakazopatikana ni upimaji wa madini, hatua itakayosaidia kuongeza thamani na ushindani wa madini hayo sokoni.

Aidha, amewataka wachimbaji na wadau wa sekta hiyo kuzingatia viwango vya ubora katika uzalishaji na usafirishaji wa madini nje ya nchi, jambo linalosaidia kuongeza faida kwao na kukuza pato la taifa.

“Bidhaa ambayo imezalishwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria za viwango, inaposafirishwa nje ya nchi huleta faida nyingi ikiwemo ongezeko la kipato,” amesisitiza.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad