MGOMBEA ubunge katika Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kaspar Mmuya amesema wananchi wa Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kura zote za ndio zinakwenda kwa mgombea urais kupitia Chama hicho Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwani amefanya maendeleo makubwa na zawadi pekee ya heshima ni kumpa tena miaka mitano.
Kwa mujibu wa Mmuya amesema Ruangwa imeguswa na maendeleo katika sekta zote muhimu sambamba na kufungua fursa za kiuchumi kupitia kilimo kutokana na Rais Samia kutoa ruzuku katika pembejeo za kilimo.
Akizungumza leo Septemba 24,2025 wakati maelfu ya wananchi wa Jimbo la Ruangwa wakiwa wamejitokeza kwa ajili ya kumpokeq mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan ,Mgombea ubunge wa hilo Mmuya ameeleza kwa kina maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wa Dk.Samia Suluhu Hassan.
“Leo wana Ruangwa tumekuwa na furaha kubwa sana ya kumpokea mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk.Samia Suluhu Hassan .Tunazo sababu nyingi za kuwa na furaha.
“Ametufanyia makubwa katika kipindi cha miaka minne tu hapa Ruangwa leo hii ukienda sekta zote za kijamii mama ameupiga mwingi.Ukienda sekta ya afya mama ameleta fedha nyingi,ameongeza vituo vya huduma za afya kutoka 34 mpaka 51.
“Zamani kulikuwa na vituo vya afya vitatu leo tunavyo 12 ,tulikuwa na zahanati 30 leo tunazo 38 ,hatukuwa na hospitali ya Wilaya lakini chini ya uongozi wa Dk.Samia tunayo,”amesema Mmuya akielezea mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Kuhusu sekta ya maji,Mmuya amesema maji ndio yanagusa uhai wa binadamu na kwa Ruangwa ambayo haikuwa na maji ya bomba leo chini ya Rais hivi sasa kila kijiji kına bomba la maji safi na salama.
“Zaidi ya hayo kuna mradi wa maj Nyangao ambapo Mama Samia ameongeza fedha nyingi kwa ajili ya kutumia chanzo hicho kuleta maji hapa Ruangwa mradi una asilimia 60 ya ujenzi. Vijiji 56 pia vitanufaika na mradi huo.
“Kwa upande wa sekta ya barabara nyie wenyewe mmekuja mpaka hapa Ruangwa hamjakanyaga vumbi mmekuja kwenye lami yenye urefu wa kilometa 52 ambazo amezitengeneza mama Samia.
“Ndani ya Wikaya hii ya Ruangwa hapa mjini kuna kilometa 18.6 ambazo ni kwa ajili ya mjini ,ndani ya kilometa hizo kuna taa 393 ili Ruangwa iwe nyeupe muda wote kwa saa 24”
Akifafanua zaidi amesema Ruangwa iko katikati hivyo chini ya Rais Dk.Samia imeendelea kuunganishwa na sasa imeunganishwa na barabara zote na bajeti ya fedha Mama Samia ameiongeza fedha .“Sasa hivi tunawekewa lami kuunganishwa na Nachingwea.Lami ya kuunganisha Lindi kupitia mandawa.”
Kwa upande wa sekta ya madini mgombea huyo wa ubunge amesema Ruangwa kuna madini ya ‘graphite’ambayo yanaweza kuchimba zaidi ya miaka 200 bila kwisha.
“Tayari mama Samia ameleta wawekezaji hapa tunawachimbaji wakubwa na wadogo hiyo itatuongezea mzunguko wa fedha na kuongeza ajira kwa vijana.
“Sisi hatuna cha kumdai mama Samia zaidi ya sisi kumpatia kura za ndio na umati huu ambao unaona hapa wamekuja kumwambia Mama ahsante kwa miaka minne na tunamhakikishia miaka mitano mingine tunampa kura zote za ndio .
“ Mimi kama mbunge ambaye ninaomba nafasi kwa mara ya kwanza nimeshawaambia Mbunge wetu na Waziri Mkuu wetu Kassim Majaliwa ambaye brute baba wa maendeleo aliongoza jimbo hili kwa miaka 15 kwa kusaidiana na Mama Samia amefanya mambo makubwa.Mipango yake yote ya kutuletea maendeleo nitaiendeleza sitaiacha
Hata hivyo amesema jambo ambalo atahakikishia analiwekea mkazo zaidi ni elimu kwa kuhakikisha kila anayeanza kusoma basi amalize elimu kwani tayari Serikali inayoongozwa na Rais Samia inatoa elimu bure.
“Sio kwamba mifumo ya elimu inashida hapana bali shida ni sisi wananchi wenyewe kwenda shuleni na kumaliza hivyo lazima mtu anayeanza shule amalize kwasababu elimu ni bure
“Lakini mama Samia amebadilisha sera ya elimu kwani hivi sasa elimu yetu kila wilaya kuna VETA na Nandagala tunayo VETA kilometa 10 kwenda kusoma.Hivyo ni lazima maendeleo ambayo tunayo tuendelee nayo kwa kuongeza mafundi zaidi.
“Nilishawaambia kila kijiji lazima tupate mafundi wasiopungua 10 wa fani mbalimbali ambao watakuwa na uwezo wa kufanya matengenezo katika sekta zote maji,umeme na miundombinu mingine ili mzunguko wa fedha uongezeke hiyo yote ni katika kukuza uchumi.
“Tunampigania Dk.Samiakwasababu hata katika ametupatia ruzuku kwa ajili ya pembejeo za kilimo lakini pia ametuwekea mfumo mzuri wa bei kwani hivi sasa wakulima tuna uhakika wa bei nzuri sokoni katika mazao ya mbaazi,korosho, ufuta na dengu.
“Nawaomba wananchi wa Ruangwa na dunia ijue sisi hatumdai chochote Dk.Samia Suluhu Hasan na sisi tunamwambia mama tutampa kura zote za ndio.”








No comments:
Post a Comment