HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 27, 2025

WAJA AREJESHA FOMU ZA UTEUZI WA UBUNGE WA JIMBO LA GEITA MJINI

Mgombea ubunge wa Jimbo la Geita Mjini,Chacha Wambura wamerudisha fomu ya uteuzi ya kugombea jimbo la Geita Mjini katika Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita,NDARO SAMSONI amepokea fomu hizo katika ofisi za tume hizo zilizopo eneo la Magogo Halmashauri ya Manispaa ya Geita. 

 

“Kwa mujibu wa taratibu wa fomu zile nne ambazo zimewasilishwa mgombea anapaswa kupewa fomu moja kwa sababu hatujafika saa 10 jioni,fomu nne tunabaki nazo na wakati tunabandika kwenye ubao wa matangazo tutampatia ile nakala yake moja na sisi tutabakia nakala tatu.”amesema Ndaro


Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kupokea fomu za uteuzi katika ofisi zote za wasimamizi wa uchaguzi nchi nzima. 

2 comments:

Post Bottom Ad